Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sekta ya viwanda
ni sehemu muhimu ya
uchumi
wa kisasa ambako
bidhaa
zinatengenezwa kwa wingi kwa kutumia
mashine
na michakato maalumu.
Viwanda huhesabiwa kati ya shughuli za sekta ya upili ya uhumi kwa jumla ambako malighafi zinabadilishwa kuwa bidhaa, kwa mfano
chuma
kuwa
feleji
na vifaa mbalimbali au
pamba
kuwa
kitambaa
na
nguo
.
Viwanda
si sehemu ya pekee ya sekta ya upili kwa mfano kuna mafundi wanaotengeneza pia bidhaa kutokana na malighafi kwa mfano wahunzi au wafumaji. Viwanda hutumia zaidi mashine, hupanga michakato yake kikamilifu na kutoa bidhaa zisizosanifishwa kwa wingi kabisa.
Aina za viwanda hutofautishwa kutokana na malighafi zinazotumia hasa kama vile
- viwanda vya kutengeneza feleji kutokana na malighafi asilia
chuma
na
makaa mawe
- viwanda vya kutengeneza bidhaa za metali kutokana na feleji kama vile mashine, magari, meli, vifaa vya umeme
- viwanda vya kemia vinavyotumia malighafi kama
mafuta ya petroli
na
minerali
pamoja na madawa mbalimbali vikitoa kwa mfano
mbolea
,
saruji
,
karatasi
,
plastiki
,
petroli
au dawa za tiba.
- viwanda vya kutolea bidhaa za matumizi ya kila siku kama vile
vyakula
, nguo,
fenicha
, magazeti, vitabu au mahitaji ya ofisi.
Viwanda kwa maana ya kisasa vimejitokeza tangu kupatikana kwa mashine hasa tangu karne ya 19. Kupatikana kwa
mashine ya mvuke
kulirahisisha gharama za kutengeneza kwa vitu na kusababisha
mapinduzi ya viwanda
yaliyoanza nchini
Uingereza
yakisambaa haraka Ulaya na Marekani.
Sekta ya viwanda ilipanua sana katika karne ya 19 hadi katikati ya karne ya 20; katika nchi zilizoendelea karibu nusu ya wafanyakazi wote walikuwa katika sekta hii. Ila tu tangu nusu ya pili ya karne ya 20 sekta ya tatu na ya nne yaani biashara na huduma zilianza kuwa na wafanyakazi wengi zaidi. Hii ni tokeo la kufanyikiwa kwa viwanda vinavyoendelea kutoa bidhaa nyingi haraka kwa kuhitaji wafanyakazi wachache kulko zamani kwa sababu uwezo wa mashine imeongezeka.
Kwa upande wa Tanzania na nchi nyingine duniani kuna viwanda vichache zaidi; hiyo inasababisha watu wengi kukosa ajira.