Sara Teasdale ( 8 Agosti 1884 – 29 Januari 1933 ) alikuwa mshairi wa kike kutoka nchi ya Marekani . Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Sarah Trevor Teasdale ; baada ya kufunga ndoa mwaka wa 1914 akatumia jina lake kama Sara Teasdale Filsinger . Mwaka wa 1918 alipokea tuzo maalumu ya Pulitzer kwa ajili ya mashairi yake.