Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
"
Salve Regina
" (tamka:?salve re?d?iːna; maana yake: 'Salamu Malkia') ni
utenzi
wa
Kikristo
unaotumika katika
liturujia
ya
Kanisa la Kilatini
hasa kama
antifona
mojawapo ya kumalizia
Sala ya mwisho
nje ya
Kipindi cha Pasaka
. Kwa kawaida unatumika pia kumalizia
sala
ya
Rozari
[1]
.
Utenzi huo ulitungwa na mtu asiyejulikana
[2]
wa
Ulaya
katika
Karne za Kati
na ulitumika kwanza kwa
lugha
ya
Kilatini
, ingawa kuna
tafsiri
zake nyingi.
- Salve, Regina, Mater misericordiæ,
- vita, dulcedo, et spes nostra, salve.
- Ad te clamamus exsules filii Hevæ,
- Ad te suspiramus, gementes et flentes
- in hac lacrimarum valle.
- Eia, ergo, advocata nostra, illos tuos
- misericordes oculos ad nos converte;
- Et Jesum, benedictum fructum ventris tui,
- nobis post hoc exsilium ostende.
- O clemens, O pia, O dulcis Virgo Maria.
[3]
- Salamu Malkia, Mama mwenye huruma,
- Uzima, tulizo na matumaini yetu, salamu.
- Tunakusihi ugenini hapa,
- Sisi wana wa Eva.
- Tunakulilia tukilalamika na kuhuzunika,
- Bondeni huku kwenye machozi.
- Haya basi, Mwombezi wetu,
- Utuangalie kwa macho yako yenye huruma.
- Na mwisho wa ugeni huu, utuonyeshe Yesu,
- Mzao mbarikiwa wa tumbo lako.
- Ee mpole, ee mwema,
- Ee mpendevu, Bikira Maria.
[4]
Utenzi huo ulipambwa kwa
muziki
na
Tomas Luis de Victoria
,
Giovanni da Palestrina
,
Josquin des Prez
,
Lassus
,
Marc-Antoine Charpentier
,
Louis-Nicolas Clerambault
,
Alessandro Scarlatti
,
Antonio Vivaldi
,
Jan Dismas Zelenka
,
George Frideric Handel
na
Franz Liszt
.
Franz Schubert
alitunga walau miziki saba tofauti. Wengine ni
Francis Poulenc
,
Arvo Part
na
Olivier Latry
.
- ↑
"
"The Rosary: Salve Regina (Hail, Holy Queen)", Godzdogz, Blackfriars, Oxford, October 2, 2014"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2020-12-02
. Iliwekwa mnamo
2022-01-16
.
- ↑
Lawrence Gushee, "Hermannus Contractus [Hermann der Lahme, Hermann von Reichenau]," in
The New Grove Dictionary of Music and Musicians
, 2nd edition (2001): "Although the most venerable ascriptions to Hermannus ? the Marian antiphons
Alma Redemptoris mater
and
Salve regina
? have been taken away by most recent scholarship, the true authorship is still, and possibly will be for ever, the subject of controversy."
- ↑
"Salve Regina"
. Preces-latinae.org
. Iliwekwa mnamo
2014-07-10
.
- ↑
Misale ya waamini
, uk. 1528.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: