Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kupasha Habari
, kadiri ya
Fra Angelico
.
Salamu Maria
(kwa
Kilatini
Ave Maria
) kwa
asili
ni
sala
ya
Wakatoliki
wa
Kanisa la Kilatini
ambayo inamsifu
Bikira Maria
na kumuomba sala zake hadi
saa
ya
kufa
.
Sala hiyo imeenea hata kwa
Wakristo
wengine, hasa
Waanglikana
, lakini kwa namna tofauti inatumiwa pia katika
Ukristo wa Mashariki
.
Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya sala hiyo inatokana na
Injili
(
Lk
1:28,42) moja kwa moja:
- Χα?ρε, κεχαριτωμ?νη, ? Κ?ριο? μετ? σο? /
Chaire, kecharit?men?, o Kyrios meta sou
/
Salamu uliyejaa neema, Bwana yu nawe
(maneno ya
Malaika Gabrieli
)
- Ε?λογημ?νη σ? ?ν γυναιξ?ν κα? ε?λογημ?νο? ? καρπ?? τ?? κοιλ?α? σου /
eulog?men? su en gynaixin kai eulog?menos o karpos t?s koilias sou
/
Umebarikiwa wewe kati ya wanawake na umebarikiwa mzao wa tumbo lako
(maneno ya
Elizabeti
)
Katikati ya
karne ya 13
sala ilikuwa inaundwa na maneno hayo tu pamoja na kuingiza
jina
la
Maria
, inavyoonekana katika
ufafanuzi
wa
Thoma wa Akwino
.
[1]
Mwishoni mwa
karne ya 15
yaliongezwa maneno ya kumuomba Maria sala zake.
[2]
Hatimaye sala kwa Kilatini imekuwa hivi:
- Ave Maria, gratia plena,
- Dominus tecum.
- Benedicta tu in mulieribus,
- et benedictus fructus ventris tui, Iesus.
[3]
- Sancta Maria, Mater Dei,
- ora pro nobis peccatoribus,
- nunc et in hora mortis nostrae. Amen.
Tafsiri ya
Kiswahili
ni:
- Salamu Maria, umejaa neema,
- Bwana yu nawe.
- Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
- na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
- Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu,
- utuombee sisi wakosefu,
- sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Salamu Maria
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|