Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Mangaliso Sobukwe
(
1924
-
1978
) alikuwa
mwanasheria
na
mwanasiasa
wa
Afrika Kusini
aliyeanzisha
Pan Africanist Congress
kupinga
ubaguzi wa rangi
nchini. Kwa ajili hiyo alifungwa kwa muda mrefu. Alikuwa muasisi wa chama hicho kilichopigania
uhuru
wa Waafrika kikijitenga kutoka kwa
African National Congress
,
pia anahusishwa na kuandaa
maandamano
ya kihistoria ya Shapeville mnamo 1960 yaliyopinga sheria ya Weusi kutembea na vitambulisho ambapo mamia ya watu waliuawa na kujeruhiwa kisha Sobukwe kuswekwa jela kunako visiwa vya Rubeni kwa miaka tisa.
Sobukwe alifariki mwaka 1978 kwa saratani na mapafu licha ya wengine kudai kuwa alipewa sumu akiwa jela.
Sobukwe alizaliwa katika eneo la Graaff-Reinet katika jimbo la
Cape Town
tarehe
5 Desemba
1924
.
[1]
akiwa
mtoto
wa mwisho katika
familia
ya kimaskini ya watoto sita.
Alisoma katika chuo cha Methodist na baadae
chuo kikuu
cha
Fort Hare University
akiwa huko ndipo alipojiunga na chama cha
African National Congress
na mwaka
1948
alichaguliwa kuwa rais wa baraza la wanafunzi .
[2]
: 420
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Robert Mangaliso Sobukwe
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|