Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
protein model mosaic.
Protini
ni
molekuli
ndefu na sehemu za lazima katika muundo wa
seli
za mwili wa
viumbehai
. Zinajengwa na
amino asidi
. Protini huwajibika kwa maumbile ya seli na kushughulika usafirishaji wa dutu ndani ya seli na kati ya seli za mwili.
Musuli
zinaundwa pamoja na protini za pekee zenye uwezo wa kupanua na kujikaza hivyo kuweka msingi wa mwendo.
Protini zinapatikana katika
wanyama
,
mimea
,
fungi
na
bakteria
.
Wanyama wote pamoja na
binadamu
huhitaji protini katika
chakula
chao kwa sababu hawana uwezo wa kujitengenezea amino asidi zote zinazohitajika kwa kujenga miili yao. Kwa sababu hiyo tunahitaji chakula chenye protini; mahitaji ya mwanadamu ni takriban
gramu
1 ya protini kwa
kilogramu
1 ya
uzito
wa
mwili
wake; maana yake mtu mwenye uzito wa kilogramu 70 anashauriwa kula gramu 70 za protini kwa siku.
Tumboni
mwa binadamu na wanyama protini za chakula huvunjwa kwa asidi asidi ndani yao; kutoka hizi mwili unajenga protini mpya ya aina yake ya pekee.
Uhaba wa protini unasababisha
magonjwa
; uhaba mkali unaleta
unyafuzi
. Unyafuzi unashika hasa
watoto
wanaopewa chakula kingi lakini
kabohidrati
tu kama
ugali
bila
makundekunde
,
nyama
au
samaki
.
Vyakula vyenye protini nyingi ni
Kando na chakula, protini huweza kupatikana katika mlo nyongeza (
diet supplements
). Kwa mfano whey protein ni mojawapo wa milo nyongeza ambao utaongeza mwili wako protini na kukuwezesha kutimua misuli.
Umuhimu wa protini katika mlo nyongeza
- Husibisha na humfanya mtu ahisi amekinai na hivi kupunguza njaa
- Hukuza misuli
- Humsaidia mtu kukuwa sawa kwa haraka baada ya mazoezi
- Hupunguza mafuta mwilini
- Kumfanya mtu awe na uzani wa kawaida
Protini zilitambuliwa na mwanakemia M
sweden
Berzelius
mwaka
1838
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
kemia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Protini
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|