Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Piramidi za Giza
karibu na
Kairo
nchini
Misri
(angalia jinsi watu na wanyama waonekana wadogo mbele ya majengo haya)
Piramidi za
Meroe
nchini
Sudan
Piramidi
(kutoka
Kigiriki cha Kale
: πυραμ?δα,
piramida
) ni kati ya
majengo
makubwa kujengwa na
binadamu
tangu zamani. Kwa jumla piramidi ni jengo lenye
msingi
wa
mraba
na
kuta
zake nne zina
umbo
la
pembetatu
zikikutana juu katikati kwenye kilele.
Ingawa
jamii
za kale katika maeneo mbalimbali ya
dunia
zilijenga piramidi, zile za
Misri
ndizo zinazofahamika na
watu
wengi
duniani
. Piramidi zimekuwa zikitumika kama kivutio kikubwa cha
utalii
kwa Wamisri; hiyo imewezeshwa na uwezo wake wa kustahimili majanga tofauti na kuzisababisha ziendelee kudumu.
Piramidi za
Misri
zilijengwa kama
makaburi
ya
wafalme
mnamo
mwaka
2000 KK
. Hasa piramidi tatu kubwa za
Giza
karibu na
Kairo
zinajulikana kote duniani zikihesabiwa kuwa kati ya "
maajabu ya dunia
" ya kale.
Piramidi za
Mesopotamia
au
zigurat
hazikujengwa kama makaburi bali kama sehemu za makaburi ikiaminiwa ya kwamba
miungu
wanakaa juu yake. Mara nyingi
Mnara wa Babeli
unaotajwa katika
Biblia
(
Mwanzo
11) umetazamwa ulikuwa zigurat.
Waindio
wa
Meksiko
, hasa
Wamaya
na
Waazteki
, walijenga pia piramidi.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Piramidi
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|
Wikimedia Commons ina media kuhusu: