Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu
(pia "ikona" kutoka
Kigiriki
ε?κ?ν,
eik?n
"
picha
" kwa kupitia
Kiingereza
icon
) kwa kawaida ni
mchoro
unaoheshimiwa ki
dini
hasa katika
Ukristo wa Mashariki
lakini pia katika
madhehebu
mbalimbali ya
Ukristo wa Magharibi
, kama vile
Kanisa la Kilatini
.
Mara nyingi picha hizo zinamhusu
Yesu
,
Bikira Maria
,
watakatifu
wengine,
malaika
na
msalaba
.
"
Sanaa ya Kikristo
" inatajwa kwanza kati ya
karne ya 2
na
karne ya 3
katika
maandishi
ya
Tertuliani
(
160
hivi -
220
) na
Klemens wa Aleksandria
(
150
hivi -
212
).
Matumizi ya picha hizo yalipingwa na baadhi ya Wakristo, hasa wa mashariki, baada ya
Uislamu
kutokea na kuenea katika maeneo yao. Hapo
kaisari Leo III
wa
dola la Roma Mashariki
alikataza picha hizo ili kujilinganisha na Waislamu na kujenga uhusiano mzuri nao.
Kumbe
wamonaki
na Wakristo wengine wengi walipinga katazo hilo. Ndio mwanzo wa mabishano makubwa yasiyoishia katika
hoja
na maandishi, bali yalichukua
uhai
wa
watu
, hasa waliodhulumiwa na
serikali
.
Hatimaye
Mtaguso wa pili wa Nisea
(
787
) ulithibitisha uhalali wa picha hizo na wa
heshima
ambazo zinapewa, kama ulivyotetewa hasa na
mtakatifu
Mwarabu
Yohane wa Damasko
.
Pamoja na kwamba picha takatifu zinasema na
mioyo
ya waamini wanyofu, mara nyingi
utaalamu
wa
ikonografia
unahitajika hasa katika kufafanua picha takatifu za
Ukristo wa Mashariki
, kwa kuwa hizo hazilengi kuiga
sura
halisi zinavyoonekana na
macho
, bali kudokeza
mafumbo
ya
imani
ili kuona yasiyoonekana.
- Beckwith, John,
Early Christian and Byzantine Art
, Penguin History of Art (now Yale), 2nd edn. 1979,
ISBN 0-14-056033-5
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Picha takatifu
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|