Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Peter Chanel.
Petro Shanel
(
12 Julai
1803
–
28 Aprili
1841
) alikuwa
padri
mmisionari
wa
Kanisa Katoliki
.
Ametambuliwa rasmi na
Papa Leo XIII
kuwa
mwenye heri
tarehe
17 Novemba
1889
, halafu na
Papa Pius XII
kuwa
mtakatifu
kama
mfiadini
tarehe
12 Juni
1954
.
Sikukuu
yake ni
tarehe
28 Aprili
[1]
.
Petro Shanel alizaliwa mjini
Cuet
,
Ufaransa
mwaka 1803.
Baada ya kupata
upadrisho
alishughulika na
uchungaji
nchini mwake kwa miaka michache, akiwajibika hasa kwa ajili ya
wakulima
na
malezi
ya
vijana
.
Halafu aliingia
Shirika la Maria
, akatumwa akatumwa katika
visiwa
vya
Oceania
pamoja na wenzake kadhaa kuhubiri
Injili
mahali ambapo ilikuwa haijatangazwa.
Licha ya matatizo mengi alifaulu kwa
upole
wake kuwaongoa watu kadhaa katika kisiwa cha
Futuna
, akiwemo
mwana
wa
mfalme
. Kwa sababu ya kuchukiwa kwa
imani
ya
Ukristo
, huyo kwa
hasira
aliagiza akamatwe na kuuawa kwa kupigwa
rungu
mwaka 1841.
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1341
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|