Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pasipoti
(kwa
Kiingereza
passport
) ni
hati
rasmi ambayo kwa kawaida inatolewa na
serikali
ya nchi na kumtambulisha
mtu
kama
raia
anayeruhusiwa kutoka na kurudi nchini. Ni hati muhimu kwa watu wanaovuka mipaka ya nchi.
Pasipoti ni
mali
ya nchi inayoitoa. Huwa na
picha
,
jina
na
sahihi
ya mtu aliyetolewa, pamoja na
tarehe
na mahali pa kuzaliwa kwake. Kuna nchi zinazoingiza pia habari za kimaumbile zinazofichwa
kielektroniki
.
Kati ya aina mbalimbali za pasipoti kuna
- pasipoti ya kawaida
- pasipoti ya
kidiplomasia
, inayotolewa hasa kwa
watumishi
waliopo kwenye
balozi
za nchi
- pasipoti rasmi inayotolewa kwa watu wengine waliotumwa na serikali au kwa niaba ya serikali ya nchi yao bila ya kuwa na hali ya kidiplomasia.