한국   대만   중국   일본 
Papa Adeodato I - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Papa Adeodato I

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papa Adeodato I.

Papa Adeodato I (pia aliitwa Deusdedit ) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Oktoba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618 [1] . Alitokea Roma , Italia [2] . Jina la baba yake lilikuwa Stephanus, ambaye alikuwa shemasi mdogo .

Alimfuata Papa Bonifasi IV akafuatwa na Papa Bonifasi V .

Kabla ya kuchaguliwa, alitoa huduma ya kipadri kwa miaka 40 [3] . Baadaye alikuza idadi ya mapadri na kuwapa nafasi zilizokuwa zimeshikwa na wamonaki kadiri ya sera ya Papa Gregori I na Papa Bonifasi IV [4] [3] .

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu [5] .

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake [6] .

Tazama pia [ hariri | hariri chanzo ]

Tanbihi [ hariri | hariri chanzo ]

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. 3.0 3.1 Attwater, Aubrey (1939). A Dictionary of Popes: From Peter to Pius XII . uk. 66. ISBN   0199295816 .
  4. Jeffrey Richards, The Popes and the Papacy in the Early Middle Ages (London: Routledge and Kegan Paul, 1979), p. 262
  5. Philips, Fr Andrew. "The Holy Orthodox Popes of Rome" . orthodoxengland.org.uk . Iliwekwa mnamo 2018-03-17 .
  6. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje [ hariri | hariri chanzo ]

Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu .
Je, unajua kitu kuhusu Papa Adeodato I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari .