Ono
ni hali inayompata
binadamu
au
mnyama
kwa ndani, lakini inajitokeza kwa nje (inaonekana). Ni tofauti na hali ya makusudi, kwa kuwa linasababishwa na jambo fulani. Ndiyo maana katika
Kiingereza
linaitwa
passion
,
neno la mkopo
kutoka lile la
Kilatini
passio
linalotokana na
kitenzi
patior
(kupatwa). Si lazima ono liwe hai, kali na tawala.
Maono ni mbalimbali, lakini yale ya msingi ni:
- upande mmoja
pendo
(kwa jambo fulani), linalosababisha
hamu
(ya jambo hilo) na hatimaye
furaha
(jambo likipatikana); upande huo pengine kuna
tumaini
na
ujasiri
;
- upande mwingine
chuki
(kwa jambo fulani), linalosababisha
hofu
(ya jambo hilo),
hasira
(dhidi ya hilo) na hatimaye
huzuni
(jambo likipatikana); upande huo pengine kuna hali ya kukata tamaa.
Kwa msingi huo,
Thoma wa Akwino
alifafanua ono kama “badiliko la
hisi
linalotokana na kukabili jema au baya la kihisi na linaloendana na tukio la kimwili katika
muundo
wake, k.mf.
pigo la moyo
”. Mabadiliko ya
utashi
ni ya
roho
tu, kumbe ono linaendana daima na tukio la kimwili kwa sababu hisi zinaendana na
viungo
.
Wanaotetea
anasa
wanasema maono yote ni maadilifu kama ustawi wa
umbile
letu; kinyume chake wengine wanayalaumu kwa kuwa yanapingana na
akili
na kuvuruga roho. Kumbe yenyewe si maadilifu wala maovu, ila yanakuwa maadilifu kadiri yanavyochochewa au kuratibiwa na akili na
utashi
yaelekee lengo adilifu. La sivyo yanakuwa maovu kwa kutolingana na akili nyofu na kulenga yasiyokubalika.
Yesu
alikusudia kuonyesha hasira takatifu alipofukuza
wafanyabiashara
hekaluni
na kupindua
meza
zao. Vivyo hivyo
bustanini
alikusudia kuwa na “huzuni nyingi kiasi cha kufa” (
Mk
14:34) ili tuelewe inavyotupasa kuhuzunikia
dhambi
zetu.
Tendo linalotumia maono kulifikia lengo adilifu linastahili zaidi, kwa kuwa
Mungu
ametujalia hisi vile alivyotujalia
kumbukumbu
,
ubunifu
na
mikono
tuvitumie kutendea mema. Kwa hiyo, “haiwezekani kutenda chema kikubwa pasipo maono” (
Blaise Pascal
), yaani pasipo hisi kuwaka
ari
ya
upendo
. Kinyume chake, maono yasiyoratibiwa yanakuwa
vilema
: pendo la kihisi linakuwa
ulafi
na
uzinifu
, chuki ya kihisi inakuwa
wivu
na
kijicho
, hofu inakuwa
woga
na
uzembe
. Hapo yanakuwa
nguvu
ya kutenda maovu badala ya kuwa nguvu ya kutenda mema.
Basi, maono hayatakiwi kung’olewa ila kuratibiwa kusudi tusiwe baridi kama watu walioganda, wala wakali kama
mito
iliyofurika. Hapo hisi zetu hazitafanana na zile za wanyama, bali zitalingana na hadhi yetu kama viumbe vyenye akili na
watoto wa Mungu
. Tufikirie hisi za Yesu zilivyokuwa kutokana na
usafi wa moyo
,
subira
na
udumifu
hata
msalabani
. Hapo tutaona jinsi hisi zetu zinavyotakiwa kuwa zaidi na zaidi chini ya akili iliyoangazwa na
imani
, chini ya utashi uliohuishwa na upendo; tena jinsi
mwanga
na
moto
hai ya
Roho
inavyotakiwa kuenea katika maono yetu ili kuyatakasa na kuyatumia kwa kumtumikia Mungu na jirani. “Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao” (
Rom
12:15).
Watakatifu
wana uwezo mkubwa ajabu wa kushiriki maono ya wenzao. Pengine wao tu wana
neno
la kuwatia moyo wenye huzuni.
Kwa hiyo tunapaswa kuratibu maono kulingana na lengo na hali. Katika nafasi ngumu tunaweza kuonja huzuni, hofu au hasira kubwa bila kutenda dhambi.
Musa
alipoona
Waisraeli
wanaabudu
ndama wa dhahabu
alikasirika na kuwaadhibu vikali (taz.
Kut
32:19-20); kinyume chake
kuhani
Eli
alihukumiwa kwa kutowakasirikia wanae (taz.
1Sam
3:11-14). Mpanda
farasi
anahitaji mara
hatamu
mara
kiboko
; vilevile ni lazima pengine kuyazuia maono, pengine kuyachochea ili kujiamsha dhidi ya uzembe,
aibu
na woga. Ni kazi ngumu kumtawala farasi mwenye nguvu, na vilevile kuratibu silika zenye uwezo wa kutenda makuu. Lakini jinsi inavyopendeza, baada ya miaka 10 au 15 ya mapambano na
nafsi
yetu, kuona tabia imebadilika na kutiwa chapa ya Kikristo!
Hasa mwanzoni mwa
maisha ya Kiroho
tusitende bila kufikiria vya kutosha, wanavyofanya wengi. Hiyo ni dhambi dhidi ya
busara
na ya
kipaji
cha
shauri
, na inatufikishia kuhukumu bila msingi: ni kama mtu anayeshuka
ngazi
haraka
mno hata akaanguka, jambo ambalo lisingetokea kama angeteremka taratibu. Tuzingatie kwanza lengo la kulifikia hadi
kazi
ya kufanya, pasipo kupuuzia yaliyopo katikati, yaani kumbukumbu ya yaliyopita, uzingatifu wa hali ya sasa,
utabiri
wa vizuio vinavyoweza vikatokea,
usikivu
wa
mashauri
muhimu. Ni lazima tuchukue
muda
ili kuamua polepole kabla hatujatenda, halafu itatupasa pengine kutenda mara moja. Lakini tukitenda kwa msukumo wa utashi au maono pasipo kuyapitia hayo tutayumba na kuanguka.
Haraka hiyo inatokana na kwamba utendaji wa kibinadamu unashika nafasi ya utendaji wa Kimungu; tunatenda kwa kuhemka, pasipo kufikiria, wala kuomba mwanga, wala kushauriwa na
kiongozi wa Kiroho
. Haraka hiyo inasababisha matendo ambayo yanakosa busara na hivyo yana matokeo ya kusikitisha. Mara nyingi inatokana na kuzingatia tu lengo la mara moja bila kuona linavyohusiana na lengo kuu linalotupasa: hapo kwa kuona tu lengo la kibinadamu tunalikusudia kwa utendaji wa kimaumbile, tusiombe vya kutosha msaada wa Mungu.
Haraka hiyo inaweza ikafanya
vijana
wenye
juhudi
watake kufikia ukamilifu mapema kuliko neema inavyowajalia, wakiruka vituo, wasizingatie hatua za katikati wala haja ya kuratibu maono. Inawatokea kama
wanafunzi
ambao mwanzoni mwa masomo wanajitahidi kutokana na upya wa mambo; lakini
udadisi
ukiisha, au juhudi zikihitajika zaidi, unafuata uzembe. Wanaingia hatari ya kudanganyika, halafu udanganyifu ukiisha, wanatumbukia uzembe na kuacha nia ya kuwajibika. Hatuwezi kufikia mara
uwiano
mzuri wa
uadilifu
. Tunapaswa kutembea
kasi
, lakini bila kupiga “hatua kubwa nje ya njia” (
Augustino
). Matokeo ya haraka hiyo ni kupoteza utulivu wa ndani na kupatwa na mafadhaiko na mahangaiko ambayo hayazai kitu ila yanafanana kijuujuu na utendaji wa kufaa.
Dawa
ni kujiweka chini ya Mungu na kulinganisha matakwa yetu na ya kwake. Hatutaridhika zaidi na nafsi zetu, ila tutaonja amani kubwa, na mara kwa mara furaha halisi ndani ya Mungu.
Ili turatibu maono tunapaswa kuepa na kupinga: upande mmoja umotomoto wa
tabia
unaoendana na kujiamini mno, upande mwingine uzembe na
uvivu
ambavyo vinaleta madhara makubwa zaidi.
Tujitafiti
kila
siku
kuhusu kazi hiyo ya polepole lakini ya daima, tukiona umuhimu wa kuratibu mwenendo wetu au, kwa usahihi zaidi, wa kudumu waaminifu kwa neema ambayo tusipokuwa nayo hatuwezi kufanya kitu kwa
wokovu
. Hapo ujasiri utasaidia
adili
la
nguvu
kutawala hofu ya kihisi. Vilevile upole utairatibu hasira itokane tu na ari ambayo ina subira bila kupotewa na umotomoto wake: hiyo ni
dalili
ya utakatifu.
- Rene Descartes,
Passions of the Soul
in J. Cottingham
et al.
eds.,
The Philosophical Writings of Descartes
Vol I (Cambridge 1985)