Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu
ya Mt. Odilone katika
Basilika
la Mt. Urban,
Troyes
,
Ufaransa
.
Odilo wa Cluny
(
962
hivi -
1 Januari
1049
) alikuwa
abati
wa
tano
wa
monasteri
ya
Kibenedikto
ya
Cluny
nchini
Ufaransa
, ambaye aliifanya kuwa muhimu kuliko zote za
Ulaya
na kuhamasisha
urekebisho
wa nyingine nyingi.
Mkali kwake mwenyewe, alikuwa mpole na mwenye
huruma
kwa wengine; kwa
jina
la
Mungu
alipatanisha
mataifa
yaliyokuwa yanapigana, wakati wa
njaa
alitegemeza kwa hali na mali wanyonge. Pia alianzisha
kumbukumbu
ya
Marehemu Wote
siku
iliyofuata
sikukuu
ya
Watakatifu Wote
[1]
.
Tangu kale anaheshimiwa na
Wakatoliki
na
Waorthodoksi
kama
mtakatifu
.
Sikukuu
yake huadhimishwa
tarehe
1 Januari
[2]
.
- ↑
Martyrologium Romanum
- ↑
Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum
, Romae 2001,
ISBN 8820972107
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|