Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wimbo/nyimbo
ni
tungo
zenye kufuata mapigo fulani ya kimi za kiafuziki yenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa
mawimbi
ya
sauti
(urari wa sauti) na mpangilio maalumu wa maneno.
Nyimbo huundwa kwa
lugha
ya mkato na matumizi ya lugha ya
picha
(taswira).
Muundo wa nyimbo huwa ni wa kuimbika na
mizani
ya kila mstari mara nyingi huwa inalingana.
Wahusika wa nyimbo huwa ni mtu mmoja au kikundi cha watu. Nyimbo aghalabu huambatana na
ala
za
muziki
kama vile
ngoma
,
zeze
,
marimba
, makofi,
vigelegele
na kadhalika.
Mashairi
ya nyimbo huimbwa popote pale panapostahili kulingana na tukio au muktadha unaofungamana na wimbo. Hivyo basi kuna nyimbo za
dini
,
harusi
,
siasa
,
jando
/
unyago
,
kilimo
, nyimbo za kuwinda na kadhalika.
- Nyimbo za wanabaharia huitwa kimai.
- Nyimbo za kulika huitwa wawe au vave.
- Nyimbo ziimbwazo mja anapofanya kazi huitwa hodiya.
- Nyimbo ziimbwazo na watoto wanapocheza huitwa Nyimbo za chekechea.
- Nyimbo ziimbwazo ili kuwabembeleza watoto huitwa bembeleza au bembezi.
Kuna aina nyingi za nyimbo zikitofautishwa na nchi,
utamaduni
na
waimbaji
wenyewe. Kwa mfano kuna nyimbo za kitamaduni, za
Kiinjili
na za kisasa.
Hivyo vikundi ni kulingana na nyakati na vinaweza kugawanywa zaidi kulingana na tofauti. Kwa mfano nyimbo za kisasa zinaweza kugawanywa kulingana na
mtindo
wa wimbo. Nyimbo zinaweza kugawanywa kulingana na nchi. Nchini
Kenya
kuna nyimbo za
makabila
tofautitofauti kama
chakacha
na
mugithi
ambazo zinahusishwa na kabila tofautitofauti.
Nyimbo za kisasa zinarekodiwa kwenye
studio
za kisasa lakini pia katika studio za nyumbani, mtindo unaoleta mageuzi makuu kwa
wasanii
. Leo unaweza kurekodi wimbo mzima ukiwa
nyumbani
mradi uwe na vifaa vinavyohitajika.
|
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Wimbo
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|