Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nikita Sergeyevich Krushchov
(
Kirusi
: Ники?та Серге?евич Хрущёв -
Nikita Sergeyevich Khrushchyov
) (
17 Aprili
1894
?
11 Septemba
1971
) alikuwa
kiongozi
wa
Umoja wa Kisovyeti
baada ya
kifo
cha
Joseph Stalin
. Alitawala kati ya
1953
hadi
1964
.
Krushchov alizaliwa mjini Kalinovka,
Urusi
. Baadaye alihamia
Ukraine
. Alikuwa mfanyakazi wa migofi akajiunga na chama cha
Bolsheviki
.
Alipanda ngazi chini ya Stalin. Baada ya kifo chake akawa kiongozi aliyemfuata. Cheo chake kilikuwa "Mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti" lakini alikuwa na madaraka kumshinda aliyekuwa na
cheo
cha rais wa nchi.
Mwaka wa 1964 aliondolewa madarakani na mfuasi wake
Leonid Brezhnev
.
Alipokuwa kiongozi alianza kufichua maovu yaliyotendewa chini ya utawala wa Stalin. Aliondoa sanamu na picha za Stalin kote Urusi na katika nchi zilizokuwa chini ya Urusi. Aliondoa maiti ya Stalin kwenye kaburi alipoonyeshwa kando la maiti ya Lenin.
Alitangaza shabaha ya kupita kiwango cha maendeleo ya Marekani lakini hakufaulu. Alijaribu kupeleka
silaha za nyuklia
katika
Kuba
lakini aliacha mipango hii alipoona kuna hatari ya vita.
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Nikita Krushchov
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|