Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nguo
ni
kitambaa
ambacho kinaweza kutumika kufunikia
meza
,
kitanda
n.k. lakini hasa kutengenezea
mavazi
mbalimbali yanayovaliwa na
mtu
kwa ajili ya kujisitiri, kwa sababu ya kutunza
heshima
yake na kujikinga dhidi ya
baridi
,
jua
,
mvua
n.k. Ndiyo sababu mara nyingi
neno
"nguo" linamaanisha mavazi yenyewe.
Nguo huvaliwa kulingana na
hali ya hewa
na
mazingira
fulani, lakini pia kulingana na
mitindo
inayobadilikabadilika kadiri ya nyakati.
Kulingana na
wanaakiolojia
na
wanaanthropolojia
, nguo za kwanza zilikuwa
manyoya
,
ngozi
za
wanyama
,
majani
na
nyasi
. Uvaaji wa nguo hizi uliwasaidia binadamu haswa katika kujikinga na
hewa
baya, kujikinga na
vumbi
pamoja na
dhoruba
kali.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Nguo
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|