Tendo la ndoa
(pia:
ngono
) ni kitendo cha kujamiiana kati ya
mwanamke
na
mwanamume
.
Jinsia
zinalenga kukamilishana katika
ndoa
. Kadiri ya
Biblia
Mungu
baada ya kumuumba
Adamu
alisema, “Si vema mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye” (Mwa 2:18).
Umbile
la
mwanamume
linaelekea kukamilishana na lile la
mwanamke
kiroho na kimwili. Lakini
roho
haionekani, hivyo ni rahisi zaidi kuona jinsi miili yao inavyofaa kuungana iwe
mwili
mmoja.
Hata hivyo tuelewe mkamilishano huo unafanyika katika
nafsi
pia, ambazo zina
vipawa
tofauti vinavyowezesha kwa pamoja kukabili vizuri
maisha
ya nyumbani, ya
uchumi
, ya
siasa
, ya
dini
n.k.
Tukiangalia
viungo vya uzazi
vya kike tunakuta kwenye kilango chake
kizinda
, yaani
nyama
nyembamba inayoondolewa na mwanamume wa kwanza anayekiingilia. Ndiyo sababu ni kama mhuri wa
ubikira
wa mwanamke. Katikati ya kizinda kuna tundu dogo tu kupitishia
damu
wakati wa
hedhi
, yaani siku zile ambazo anatokwa damu kupitia
uke
ulio nafasi ya wazi (kati ya kizinda na
tumbo la uzazi
) iliyo tayari kupokea
uume
na
mbegu
zake.
Hizo zinasafiri muda wa saa sita hivi katika tumbo la uzazi ili kukifikia
kijiyai
katika
mrija
unaoliunganisha na
kifuko cha kijiyai
. Mbegu zinazofunga safari hiyo zinaweza kuwa milioni kadhaa, lakini chache tu zitafika; tena kati yake, moja tu itapenya kijiyai, kwa sababu mara tu inapoingia kijiyaji kinakuwa kigumu kwa nje, hivi kwamba mbegu nyingine zitagonga bure. Ikiwa mbegu hiyo inabeba
kromosomu Y
mtoto
atakuwa wa kiume, la sivyo atakuwa wa kike.
Mbegu na kijiyai vinapounganika,
viini vya urithi
vinavyobebwa navyo vinachanganyikana kwa namna mojawapo kati ya zile zote zinazowezekana. Kwa kawaida viini hivyo ni 46 kwa kila
binadamu
, na kila
seli
ya mwili wake inavyo. Katika viini hivyo zimo
jeni
25,000 hivi, yaani sifa zote za mtu huyo maalumu tangu atungwe hadi afe.
Viini hivyo vinaongoza ujenzi wa mwili kwanza tumboni mwa mama, halafu utengenezaji wa seli mpya baada ya kuzaliwa. Hata mbegu zote zina viini hivyo vya
baba
, na vijiyai vyote vina viini hivyo vya
mama
, isipokuwa katika kukomaa vinapungua na kubaki 23 tu kusudi mbegu na kijiyai vikiungana
mimba
inayopatikana iwe na viini 46 kama kawaida.
Kutokana na wingi usiohesabika wa namna ambazo jeni hizo zinaweza kuchanganyikana, hakuna mtu aliye sawa na mwingine, kama vile
alama za vidole
zilivyo tofautitofauti. Hivyo toka mwanzo mimba hiyo ni mtu wa pekee, ingawa ina seli moja tu. Seli hiyo itakua na kuanza kugawanyika katika seli 2, 4, 8, 16 n.k.
Ingawa kila moja ina viini vilevile, polepole seli zinatofautiana ili kufanya kazi maalumu (
ubongo
,
moyo
na
viungo
vingine) na kushirikiana zote vizuri katika umoja wa mwili. Baada ya miezi miwili viungo vyote vimeshatengenezwa, halafu vinazidi kukua na kukamilika hadi mwezi wa tisa ambapo mwishoni mwake mtoto atazaliwa.
|
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Tendo la ndoa
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|