Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ngome ya Yesu
mjini
Mombasa
ni mfano mashuhuri wa ngome katika
Afrika ya Mashariki
.
Ngome
(kwa
Kiingereza
castle, fort
) ni
jengo
kubwa lililoimarishwa kwa shabaha ya kujihami dhidi ya maadui na kujitetea dhidi ya mashambulio.
Kutokana na
maendeleo
ya
teknolojia
ya
silaha za moto
ngome hazitumiwi tena kwa kusudi hizi. Lakini ngome nyingi
duniani
zimebaki kama ushuhuda wa kihistoria wa
karne
zilizopita. Ilhali ngome zilijengwa kwa
kuta
nene na muundo imara, mabaki yao yamedumu miaka mingi.