Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera ya nasaba ya Qing (1890?1912)
Eneo la China chini ya nasaba ya Qing mnamo 1820
Nasaba ya Qing
(
Kichina
: ?朝;
pinyin
: Q?ng chao) ilitawala
China
kati ya
1644
na
1912
.
Watawala wa Qing walichukua nafasi ya ma
kaisari
wa
nasaba ya Ming
. Familia ya Qing ilitoka
Manchuria
na kwa sababu hii huitwa pia "Nasaba ya Manchu".
Chanzo cha watawala kutoka Manchuria
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mnamo
1580
BK
Mmanchuria
Nurhaci
alikuwa jenerali wa kitengo cha kaskazini cha jeshi la nasaba ya Ming. Nurhaci aliunganisha makabila ya Wamanchuria na tangu
1616
akajiita
Khan
wa Manchuria yote.
Kuanzia 1644 jeshi la Wamanchuria lilianza kuvamia sehemu kubwa za China ya kaskazini na kupindua nasaba ya Ming.
Walihamisha mjiu mkuu wao kwenda Beijing.
Karne za utawala wa Qing zilileta maendeleo makubwa katika uchumi na idadi ya wakazi wa China iliongezeka kutoka watu milioni 143 mnamo 1740 hadi watu milioni 430 mnamo 1850. Serikali ilisimamia karahana za mafundi waliotenegeneza bidhaa nyingi zilizopelekwa hadi Ulaya na Marekani. China ilikuwa na mapatao makubwa ya dhahabu kutoka Ulaya kutokana na biashara hii. Kati ya bidhaa zilizotafutwa Ulaya zilikuwa hasa vyombo vya
kauri
,
fanicha
na kazi za sanaa.
Ugomvi na Uingereza na vita ya afyuni
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kuanzia miaka ya 1820 Waingereza waliongeza biashara ya afyuni katika China. Majaribio ya serikali ya Qing kusimamisha biashara ya dawa hili la kulevya likasababisha
vita ya afyuni
ya kwanza (1839 bis 1842) ambako manowari za Uingereza zilishinda wanajeshi wa maji Wachina na kuteka niji muhimu kwenye pwani. Chini ilipaswa kukubali amani iliyoruhusu biashara ya afyuni na kuondoa masharti mengine kuhusu biashara ya nje.
Kwa njia hii China ya Waqing haikuwa tena nchi huru lakini ilipaswa kuwapa wageni kutoka Ulaya nafasi kubwa na kubwa zaidi katika biashara na uchumi. Pamoja na hayo mataifa ya Ulaya yalitwaa miji kama Hongkong kama vituo vyao vya kibiashara na kijeshi.
Mwisho wa Qing na ufalme katika China
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mwisho wa karne ya 19 vikundi mbalimbali ndani ya nasaba ya Qing walianza kuvutana juu ya matengenezo ya utaratibu wa kijamii na kisiasa.
Malkia Cixi
alizuia mabadiliko haya. Hadi kifo chake mwaka 1908 alitawala China iliyoendelea kushuka katika hali ya nusukoloni ya nchi za Ulaya. Kabla kifo chake alimteua mtoto
Pu Yi
kama kaisari mpya lakini utawala wa Qing ilipinduliwa katika
mapinduzi ya China ya 1911
iliyomaliza nasaba ya Qing pamoja na ufalme katika China. Pu Yi alilazimishwa kuachana na cheo cha Kaisari mwaka 1912.
Mwaka 1934 hadi 1945 Japani ilimteua kama mtawala wa
Manchuria
iliyokuwa nchi kwa jina tu chini ya usimamizi wa Japani.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Nasaba ya Qing
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|