Mwanamke
ni
mwanadamu
wa
jinsia
ya kike, kwa maana anafaa kuwa
mke
. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia
utu uzima
au walau ame
balehe
.
Kabla ya hapo huwa anaitwa
mtoto
wa kike, binti, mwanamwali au
msichana
.
Baada ya kuzaa anaitwa kwa kawaida
mama
,
jina
lenye
heshima
kubwa katika
utamaduni
wa aina nyingi.
Akianza kupata
wajukuu
, anajulikana pia kama
bibi
.
Wanawake ni takriban
nusu
ya binadamu wote, wengine huwa
wanaume
. Ndizo jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.
Mwanamke ana
tabia
zake za pekee upande wa
mwili
,
nafsi
na
roho
, na tofauti kati yao na
wanaume
hujitokeza kwa namna mbalimbali katika
utendaji
.
Katika maumbile ya
mwili
wanawake huwa na
viungo vya uzazi
vya kike ambavyo ni vya pekee na kulindwa kwa jumla ndani ya mwili.
Msingi wa tofauti hizo ni hasa
chembeuzi
cha jinsia, yaani wanaume wana
jozi
la
chembeuzi "X"
na
"Y"
ndani ya
seli
zao zote, lakini wanawake wana jozi la "X" mbili. Chembeuzi Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.
Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanawake kuwa tofauti na wanaume. Kuna pia tabia za kiakili na za kiroho za pekee zinazoonekana wazi kati ya wanawake wengi.
Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia
utamaduni
kwa sababu mara nyingi watu wamepanga
shughuli
na pia namna ya
maisha
tofauti kwa wanaume na wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua ma
tokeo
ya mapatano hayo kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.
Pamoja na hayo, kuna wanawake wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kiume. Sababu kuu ni kwamba miili yao huwa na viwango vya homoni tofauti na kawaida. Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kike wanaojisikia kuwa wanaume, pengine kutokana na matukio ya utotoni au athari nyingine za
kisaikolojia
.
Tazama pia
Marejeo
- Chafe, William H.
Archived
13 Januari 2009 at the
Wayback Machine
., "The American Woman: Her Changing Social, Economic, And Political Roles, 1920?1970", Oxford University Press, 1972.
ISBN 0-19-501785-4
- Roget’s II: The New Thesaurus
, (Boston: Houghton Mifflin, 2003 3rd edition)
ISBN 0-618-25414-5
- McWhorter, John. 'The Uses of Ugliness',
The New Republic Online
, January 31, 2002. Retrieved May 11, 2005 ["bitch" as an affectionate term]
- McWhorter, John.
Authentically Black: Essays for the Black Silent Majority
(New York: Gotham, 2003)
ISBN 1-59240-001-9
[casual use of "bitch" in ebonics]
- Routledge international encyclopedia of women
, 4 vls., ed. by Cheris Kramarae and Dale Spender, Routledge 2000
- Women in world history : a biographical encyclopedia
, 17 vls., ed. by Anne Commire, Waterford, Conn. [etc.] : Yorkin Publ. [etc.], 1999?2002
Viungo vya nje
- Historia
- Dini
|
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mwanamke
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|