Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muda
ni kipindi ambacho mtu aidha alifanya, anafanya au anatarajia kufanya jambo fulani. Katika
maisha
tumepitia vitu mbalimbali, baadhi tunaweza tukavikumbuka na vingine hatuvikumbuki, na katika maisha kadri muda unavyokwenda ndivyo vitu vinazidi kugunduliwa kutokana na ongezeko la
sayansi
.
Katika
maisha
ya kila siku
mwanadamu
hutegemea sana muda ili kufanikisha malengo yake.
Muda hutumika na watu mbalimbali kwa mambo mbalimbali kama itakavyoelezwa hapa chini:
- mwanafunzi
hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujisomea.
- mfanyakazi
hutumia muda wake hasa kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.
Endapo watautumia muda huo vibaya, hakika hawataweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Hata hivyo ni muhimu kuwa na uwiano mzuri katika matumizi ya muda, kwa mfano, kwa
sala na kazi
.