Msitu wa mvua
ni
msitu
unaopokea mvua nyingi yaani
usimbishaji
wa zaidi ya
milimita
2,000 kwa mwaka. Kwa hiyo msitu unastawi vizuri kuna aina nyingi za
mimea
na wanyama kushinda misitu mingine.
Kuna namna mbili za misitu hii kutokana na
halijoto
:
- Misitu ya mvua ya kitropiki katika nchi za joto
- Msitu wa mvua penye
tabianchi
ya wastani.
Misitu hii iko kwenye kanda ya ikweta
duniani
kati digrii za
longitudo
10° kusini na kaskazini.
Maeneo makubwa yako hasa
Brazil
katika beseni ya
Amazonas
, Afrika katika beseni ya
mto Kongo
,
Asia ya Kusini-Mashariki
na kaskazini ya
Australia
.
Misitu hii imepungua sana kutokana na kukatwa kwa miti na upanuzi wa kilimo.
Misitu ya mvua penye tabianchi ya wastani
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Nje ya kanda ya tropiki kuna misitu ya mvua kwenye pwani la magharibi ya
Amerika Kaskazini
,
Chile
,
Tasmania
,
New Zealand
,
Japani
na kwenye magharibi ya
Kaukazi
.
Ardhi na matatizo ya kilimo cha kisasa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Misitu ya mvua huonyesha rutba kubwa lakini ardhi yenyewe mara nyingi inakosa rutba.
Hii ni sababu ya kwamba maeneo ya misitu ya mvua hayafai kwa kilimo. Kama miti inakatwa mvua nyingi huondoa minerali za ardhi na kuzipeleka mtoni. Ardhi yenyewe inachoka haraka na baada miaka michache mavuno hupungua kabisa. Hii imeonekana mahali pengi ambako maeneo ya misitu hii yaligeuzwa kuwa mashamba; baada ya miaka michache ya mavono mazuri wakulima waliopata shida ya kudumisha maisha yao. Kwa bahati mbaya mara nyingi wakulima wale wameendelea kukata miti zaidi wakiacha nyuma kanda la nusu-jangwa.
Wenyeji asilia waliolima katika misitu hii walitumia maeneo madogo madogo tu wakihamahama hivyo mashamba yao yalifunikwa kirahisi tena na miti ya karibu iliyozuia uharibifu wa ardhi.
Miti na mimea inastawi vizuri kwa sababu majani pamoja na ubao wa miti inayoanguka chini na maiti za wanyama vinaoza katika unyevu haraka na kuwa chakula cha mimea tena. Harakati hii inasaidiwa na aina nyingi za uyoga zinazosaidia kuozesha haraka vitu vyote vyenya asili ya mimea au wanyama.
Imekadiriwa ya kwamba zaidi ya nusu, labda theluthi mbili za spishi zote za mimea na wanyama duniani hupatikana kwenye misiti ya mvua. Mamilioni ya spishi hazikutambuliwa bado.
Misitu ya mvua ya kitropiki imeitwa "duka la madawa ya dunia" kwa sababu kiasi kikubwa cha dawa asilia kutokana na mimea imepatikana hapo.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Msitu wa mvua
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|