Mohamed Said
|
Nyuma wapili Bakari Saleh, mwisho kulia
Ilunga Hassan Kapungu
,
Mstari wa mbele watatu kutoka kushoto Mwanahistoria - Mwandishi Mohamed Said. Hawa walikuwa baadhi ya vijana wa Kiislamu waliohudhuria Semina Dodoma
Chuo Cha Biashara 1988.
|
Amezaliwa
|
25 Februari
1952
(
1952-02-25
)
(umri 72)
Gerezani
,
Dar es Salaam
|
Nchi
|
Tanzania
|
Kazi yake
|
Mwandishi, mwanahistoria
|
Mohamed Said Salum
(alizaliwa
Gerezani
,
Dar es Salaam
,
25 Februari
,
1952
) ni
mwandishi
na
mwanahistoria
kutoka nchini
Tanzania
. Ametunga
vitabu
mbalimbali, lakini anafahamika zaidi kwa kitabu chake cha "
Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes
" kilichotolewa kwa
lugha
ya
Kiingereza
kwa mara ya kwanza
1998
. Baadaye kikatafsiriwa kwa
Kiswahili
na kutolewa tena mnamo
mwaka
2002
.
Sheikh Mohamed Said Abdallah alizaliwa mnamo tarehe
25 Februari
katika mwaka wa
1952
huko
Gerezani
jijini
Dar es Salaam
- ambapo ndiko kulikokuwa na
asili
ya upinzani dhidi ya
ukoloni
wa
Waingereza
katika
Tanganyika
. Babu yake, Mzee Salum Abdallah Popo alikuwa muasisi wa harakati za vyama vya wafanyakazi na alikuwa mmoja kati ya watu wa awali kabisa kuanzisha upinzani na kuunga mkono hoja ya kupinga utawala wa kikoloni. Mwaka wa 1947, Mzee Popo aliongoza mgomo wa kwanza nchini
Tanganyika
katika majimbo ya kati nchi uliopangwa na wafanyakazi wa Tanganyika Railways.
Tanganyika ilipopata uhuru wake mwaka 1961, Mzee Popo aliachana na mkono wa
Nyerere
kama jinsi wengi walivyofanya na alitiwa kizuizini na serikali kwa ajili ya msimamo wake wa kuwa vyama vya wafanyakazi sharti viwe huru. Akiwa mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU) alipinga vyama vya wafanyakazi kuwekwa chini ya
Tanganyika African National Union
(TANU) chini ya Rais Julius Nyerere.
Sheikh Mohamed Said ana shahada katika masuala ya Sayansi ya Siasa kutoka katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
. Vilevile ana Stashahada katika masuala ya Maritime Studies kutoka katika
Chuo Kikuu cha Wales
huko mjini
Cardiff
,
Wales
na nyingine ya BIMA kutoka katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha Dar es Salaam (IFM).
Utafiti juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Mohamed Said amefanya utafiti mwingi sana juu ya historia ya uhuru wa Tanganyika, historia ambayo kabla ya utafiti wake ilichukuliwa kama iliyohitimishwa na ameweza kufukua mambo muhimu ambayo yalifichwa katika historia iliyokuwa ikitambulikana rasmi.
Alianza kufahamika zaidi katika miaka ya themanini kupitia makala zake za kusisimua zilizokuwa zinahangaisha fikra za wasomaji kwa kufichua yale yaliyofichwam zilizoelezea mchango muhimu wa Waislamu na Uislamu katika harakati za kupinga ukoloni katika Tanganyika na khiyana waliofanyiwa Waislamu na serikali zote mbili, yaani, kabla ya uhuru na baada ya uhuru - jambo ambalo kwa wakati ule lilikuwa mwiko kufanyiwa utafiti au kuandikwa.
Makala hizo zilipata kuchapishwa katika magazeti na majarida maarufu barani Afrika na katika magazeti ndani na nje ya Tanzania. Baadhi tu ya makala zake za utafiti ni pamoja na "In Praise of Ancestors" (1988), "Africa Events (London), "Abdulwahid Sykes: Founder of a Political Movement" Africa Events - London (1988), "Islam and Politics in Tanzania" (1989), Al Haq Internation (Karachi), "The Plight of Tanzania Muslim" (1993) Change (Dar es Salaam) na "The Secular Unsecular State" (1995) Change (Dar es Salaam).