Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mahali pa mkoa wa Sistan na Baluchistan katika Uajemi
Sistan na Baluchistan (
kaj
??????? ? ?????????) ni moja wa mikoa 30 ya
Uajemi
. Makao makuu yako mjini
Zahedan
.
Mwaka 2006 idadi ya wakazi ilikuwa watu 2,405,742. Mkoa una eneo la 181,785
km²
na msongamano wa wakazi 13 kila kilomita ya mraba.
Mkoa uko katika kusini mashariki ya Uajemi ukipakana na
Afghanistan
,
Pakistan
,
Ghuba ya Omani
(
Bahari Hindi
) na mikoa jirani ya
Khorasan Kusini
,
Kerman
na
Hormozgan
.
Zahedan yenye wakazi 567,449 (sensa 2006) ni mji mkubwa mkoani. Kaskazini ya mkoa ni eneo la Sistan na kusini ya mkoa ni sehemu ya kiajemi ya
Baluchistan
.
Mkoa hupokea
mvua
kidogo kwa wastani milimita 80 kwa mwaka. Sehemu kubwa ya
usimbishaji
hupatikana kati ya Oktoba na Machi ( mvua milimita 8 - 15) na miezi kati ya Aprili na Septemba ni yabisi yenye usimbishaji wa milimita 0 - 8 pekee.
Halijoto ya wastani ni
sentigredi
20.8; mwezi baridi ni
Januari
yenye wastani ya 7.5
°C
na mwezi wa joto ni
Julai
yenye wastani ya 33.1 °C.
Sistan na Baluchistan huwa na wilaya 8 ambazo ni
Wakazi walio wengi sana ni
Wabaluchi
ambao ni jamii kubwa yenye lugha ya pamoja wanaokalia sehemu za Uajemi mashariki, Afghanistan kusini na kusini-magharibi ya Pakistan.
Wengi wao ni
Wasunni
tofauti na wakazi wengine wa Uajemi walio
Washia
hasa.
Umaskini ni kubwa mkoani ingawa kuna malighafi kama madini mbalimbali ambazo hazikuanza kuchimbwa bado.