Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkate wa uzima
(kwa
Kigiriki
?ρτο? τ?? ζω??,
artos t?s z??s
) ni mojawapo kati ya namna
saba
ya
Yesu Kristo
kujitambulisha katika
Injili ya Yohane
kwa kutanguliza "Mimi ndimi..."
[1]
.
Yesu
alijiita hivi baada ya kuzidisha
mkate
na
samaki
kwa
umati
wa
watu
waliomfuata.
Lengo la
muujiza
huo halikuwa tu kutuliza
njaa
yao, bali kudokeza
karamu
ya
mbinguni
ambayo itashibisha
hamu
zote za
binadamu
kwa utimilifu wa
uzima
.
Hotuba
hiyo inapatikana katika
Yoh
6:22-59 ambamo imeandikwa kuwa ilitolewa katika
sinagogi
la
Kapernaumu
.
[2]
Pamoja na kwamba
Injili
hiyo haisimulii jinsi Yesu alivyowaachia
wanafunzi
wake
mwili
na
damu
yake katika
maumbo
ya mkate na
divai
wakati wa
karamu ya mwisho
, inazungumzia
fumbo
la
ekaristi
hasa katika sehemu ya mwisho ya hotuba hiyo, ikisisitiza kuwa Yesu amejifanya
chakula
kweli na
kinywaji
kweli
[3]
.
Kwa njia yake tu mtu anaweza kuwa na
uzima wa Kimungu
(Yoh 5:26)
[4]
.
- ↑
Who Do You Say That I Am?: Essays on Christology
by Jack Dean Kingsbury, Mark Allan Powell, David R. Bauer 1999
ISBN 0-664-25752-6
page 83
- ↑
The Gospel According to John: A Literary and Theological Commentary
by Thomas L. Brodie 1997
ISBN 0-19-511811-1
page 266
- ↑
The Eucharist in the New Testament
by Jerome Kodell 1988
ISBN 0-8146-5663-3
page 118
- ↑
The Person of Christ
by Gerrit Cornelis Berkouwer 1954
ISBN 0-8028-4816-8
page 163
|
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mkate wa uzima
kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|