Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Misri ya Kale
ni
ustaarabu
uliokuwepo
Afrika kaskazini
, sambamba na mto
Naili
, kuanzia kwenye
delta
au
mdomo
wa Naili, toka
kaskazini
mwa
Misri
kwenda
kusini
hadi
Jebel Barkal
, kwenye
maporomoko
ya nne, wakati wa kupanuka kwake (
Karne ya 15 KK
).
Ustaarabu huo ulidumu kwa karibu
milenia
tatu, toka takribani mwaka
3200 KK
hadi mwaka
30 KK
nchi ilipovamiwa na
Waroma
na kuwa sehemu ya
Dola la Roma
. Historia ya kisiasa hutazamwa kuanza na
Farao Menes
mnamo
3200 KK
na kwisha na
uvamizi
wa
Wagiriki
chini ya
Aleksander Mkuu
mnamo
332 KK
. Kinachofuata kilikuwa kipindi cha Misri kama nchi ya kujitegemea chini ya
mafarao
Wagiriki (
nasaba ya Ptolemaio
) hadi kuvamiwa na Waroma na kuwa
jimbo
la Dola la Roma.
Uti wa mgongo
wa Misri ya Kale ulikuwa mto Naili. Sehemu kubwa ya nchi hiyo ni
jangwa
lakini
umwagiliaji
wa
mashamba
kwa njia ya
maji
ya mto huo ulileta
mazao
mazuri yaliyolisha watu wengi.
Mahitaji ya kupanga na kutunza
mifereji
pamoja na mitambo ya umwagiliaji na kusimamia ugawaji wa maji yalisaidia kutokea kwa vyanzo vya
hisabati
na
mwandiko
.
Mwandiko
wa Misri ulikuwa
hiroglifi
zilizokuwa aina ya mwandishi wa
picha
.
Dini
ya Misri ilitarajia
maisha
baada ya
kifo
ambayo yanapaswa kuandaliwa na watu wakati wa maisha haya.
Wafalme
, walioitwa Ma
farao
, walijengewa
makaburi
makubwa sana na
piramidi
zao ni kati ya makaburi makubwa kabisa
duniani
.
Vipindi vya historia ya Misri ya Kale
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Historia ya Misri hugawiwa kufuatana na
nasaba
za wafalme wake ambao kwa jumla zilikuwa 31. Kuna ugawaji wa kimsingi kwa vipindi vikuu vitatu:
- Himaya ya Kale ya Misri (3200 KK - 2100 KK)
- Himaya ya Kati ya Misri (2100 KK - 1500 KK)
- Himaya Mpya ya Misri (1500 KK - 332 KK)
Siku hizi wanahistoria wamezoea ugawaji wa undani zaidi, ilhali miaka ya kuanza na kuishia mara nyingi hayana uhakika.
- Historia ya awali ya Misri: 4000 KK hivi
- Kipindi kabla ya maungano ya Kusini na Kaskazini: ca. 4000 KK ? 3100 KK
- Kipindi cha nasaba za kwanza: 3100 KK? 2700 KK (nasaba 1 na 2)
- Himaya ya Kale: 2686 KK ?2181 KK (nasaba ya 3 ? 6)
- Kipindi cha kwanza cha mpito: 2216?2137 KK hivi (nasaba ya 7 - 11)
- Himaya ya Kati: 2137?1781 KK hivi (nasaba ya 11 - 12)
- Kipindi cha pili cha mpito: 1648?1550 KK hivi (nasaba ya 13 ? 17)
- Himaya Mpya: 1550?1070 KK hivi (nasaba ya 18 ? 20)
- Kipindi cha tatu cha mpito: 1070?664 KK hivi (nasaba ya 21 - 25)
- Kipindi cha mwisho: 664?332 KK hivi (nasaba ya 26 ? 31)
- Kipindi cha Wagiriki: 332 KK - 395 n. Chr (nasaba ya Ptolemayo)
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Misri ya Kale
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|