Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Michelle LaVaughn Obama
(jina la kuzaliwa ni
Michelle LaVaughn Robinson
; alizaliwa
17 Januari
1964
) ni
Mwanasheria
wa
Marekani
na ndiye
mke
wa aliyekuwa
Rais
wa Marekani,
Barack Obama
.
[1]
Huyu ndiye wa kwanza mwenye asili ya
Afrika
kuwa mke wa Rais wa Marekani.
Michelle alizaliwa na kukua katika kitongoji cha
South Side
ya
Chicago
na kusoma hadi kuelekea katika
Chuo Kikuu cha Princeton
halafu katika
Kitivo cha Sheria cha Harvard
.
Baada ya kumaliza elimu yake hiyo, alirudi Chicago na kukubali kuchukua nafasi ya kazi katika kampuni ya Sidley Austin, halafu akaja kuwa mmoja kati ya wafanyakazi wa meya wa Chicago Richard M. Daley, halafu baadaye akafanya kazi katika
Chuo Kikuu cha Chicago
na Hospitali za Chuo Kikuu cha Chicago.
Michelle Obama ni dada wa Craig Robinson, kocha wa mpira wa kikapu wa Oregon State University. Alikutana na Barack pale alipojiunga na Sidley Austin. Pale Barack Obama alipochaguliwa kuwa kama Seneta, familia ya Obama ikachagua kuishi mjini Chicago South Side kuliko kuishi mjini
Washington, D.C.
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Michelle Obama
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|