Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Katika
wikipedia
hii tunatumia neno "mbingu" zaidi kwa maana ya kidini. Kwa mbingu kama uwazi tunaoona juu ya uso wa
ardhi
penye ma
wingu
,
jua
na
nyota
tazama
anga
Mbingu
ni upeo wa
Mungu
au
miungu
katika mafundisho ya
dini
nyingi. Mara nyingi humaanisha pia upeo wa kiroho ambako
nafsi
za wafu huweza kufikia baada ya
kifo
.
Watu walioishi zamani, wakitegemea
macho
yao pekee, waliona mara nyingi ya kwamba mbingu ziko juu yetu, na tukitazama
anga
tunaona mwanzo wa mbingu kama mahali pa Mungu.
Lakini tangu kale watu wengine waliona ya kwamba mbingu si mahali maalumu, bali zaidi hali au upeo ambao ni tofauti na mahali popote tunapojua au tunapoweza kutambua.
Katika
lugha
ya kila siku maneno "
anga
" na "mbingu" mara nyingi yanatumiwa kwa maana moja: "Ma
wingu
yanatembea angani - mawingu yanatembea mbinguni".
Lakini mbingu huwa na maana ya ziada, yaani ya kidini, kwa kutaja pia upeo wa Mungu au hali inayopita maarifa ya
duniani
: "hapa ninajisikia kama mbinguni" ni tofauti sana na "hapa najisikia angani".
Kiasili "mbingu" ni uwingi wa neno "uwingu"
[1]
ambalo si kawaida sana tena. Uwingu linataja uwazi juu yetu, ni upeo wa
mawingu
. Mbingu kama uwingi wake unatokana na dhana la kuwepo kwa tabaka mbalimbali za uwingu huu, hivyo mbingu. Mataifa ya kale yaliamini kuweko kwa mbingu saba kwa sababu waliona mianga saba angani yaliyokuwa na mwendo kati ya nyota yaani
Jua
,
Mwezi
na sayari tano zilizojulikana kabla ya kupatikana kwa darubini (
Utaridi
,
Zuhura
,
Mirihi
,
Mshtarii
na
Zohali
). Hapa waliwaza kuwepo kwa mbingu saba ilhali kila moja alikuwa na tabaka yake ya uwingu. Kupitia maandiko ya Waislamu mtazamo huu wa dunia ulisambaa katika nchi nyingi hadi Uswahilini.
- ↑
Charles Sacleux
, Dictionnaire Swahili- Francais, Paris 1939, makala "uWingu"
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|