Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa plural ya ziwa, tazama
Ziwa
.
Maziwa
ni
kiowevu
cheupe kinachotolewa na majike wa
mamalia
kama
lishe
kwa ajili ya
watoto
wao.
Wanyama
wadogo hulishwa maziwa katika miezi ya kwanza ya
maisha
yao hadi kuzoea
chakula
cha kawaida.
Nje ya lishe ya wanyama changa, maziwa hutumiwa na
binadamu
kama
kinywaji
na
chakula
. Watu hufuga wanyama wanaotoa maziwa, hasa
ng'ombe
, kwa kusudi la kukamua maziwa yao. Wanyama wengine wanaofugwa na kukamuliwa kwa maziwa yao ni
mbuzi
,
kondoo
na
ngamia
,
farasi
,
punda
na
nyati
.
Maziwa hunywewa au kuungwa katika upishi wa chakula. Tatizo la matumizi ya maziwa ni ya kwamba yanabadilika haraka. Inakamuliwa pamoja na
vidubini
ndani yake na pia vidubini vilivyomo
hewani
hupenda kuingia ndani yake kwa sababu maziwa yana lishe nyingi. Vidubini hivi vinasababisha kuchachuka kwa maziwa; mara nyingi
ladha
inaweza kubadilika kwa namna isiyotakiwa.
Kwa hiyo maziwa yanayotolewa kwenye
viwanda vya maziwa
hupata
upasteurishaji
na hutunzwa kwenye
baridi
chini ya kiwango cha
sentigredi
7. Katika
mazingira
asilia maziwa yaliyochachuka hunyewa au, kama yameganda, huliwa.
Katika nchi nyingi maziwa hugandishwa na kukaushwa kuwa
jibini
. Maziwa katika
umbo
la jibini hutunzwa muda mrefu na ni chakula bora. Njia nyingine ya kutunza maziwa ni kuondoa
maji
ndani yake kabisa na kutunza
unga la maziwa
.
Mafuta
ya maziwa hutolewa mara nyingi kuwa
krimu
au
siagi
.