Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Masifu ya jioni
ni kipindi muhimu zaidi cha
Sala ya Kanisa
katika
madhehebu
mbalimbali ya
Ukristo
.
[1]
[2]
Ni
sala
rasmi inayofanyika wakati wa
jua
kuelekea kutua ili kumshukuru
Mungu
kwa
siku
inayokaribia kwisha.
[3]
Katika
utaratibu
wa
Kanisa la Roma
, unaofuatwa na
majimbo
karibu yote ya
Kanisa Katoliki
la Kilatini
, sehemu kuu za sala hiyo, kati ya utangulizi na
baraka
ya mwisho, ni
utenzi
,
zaburi
mbili (au moja ndefu iliyogawiwa pande mbili),
wimbo
kutoka
Nyaraka
za
Mitume
au
kitabu cha Ufunuo
,
somo
fupi au refu kutoka
Agano Jipya
,
kiitikizano
,
wimbo wa Bikira Maria
,
maombezi
,
Baba Yetu
na sala ya kumalizia.
Kati ya sehemu hizo,
kilele
ni maneno ya
Injili
(wimbo wa Bikira Maria na Baba Yetu).
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Masifu ya jioni
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|