Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mark Richard Shuttleworth
(*
18 Septemba
1973
) ni
mjasiriamali
kutoka nchini
Afrika Kusini
aliyekuwa
Mwafrika
wa kwanza kufika kwenye
anga-nje
.
Alizaliwa
mwaka
1973 kwenye
Dola Huru la Oranje
akiwa
mtoto
wa
daktari
na
mwalimu
. Baada ya kumaliza
shule
1991
alisoma
biashara
kwenye
Chuo Kikuu cha Cape Town
akapokea
digrii
ya kwanza mwaka
1996
.
Wakati bado alikuwa
mwanafunzi
alishiriki kwenye ukuzaji wa
programu
ya Debian, nakala moja ya
Linux
.
Mwaka
1995
aliunda
kampuni
ya Thawte Consulting iliyokuza programu za usalama wa
intaneti
. Mwaka
1999
aliuza kampuni yake kwa
dolar
milioni
575 kwa kampuni ya
Marekani
Verisign
[1]
.
Mwekezaji katika programu huria
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Miaka iliyofuata aliwekeza
pesa
kwenye miradi mbalimbali inayolenga kusaidia wajasiriamali wapya. Mwaka
2001
aliunda Taasisi ya Shuttleworth inayosaidia miradi ya kuboresha
jamii
ya Afrika Kusini, hasa miradi huria ya intaneti inayojenga
elimu
[2]
.
Tangu mwaka
2005
Shuttleworth alijishughulisha na programu
dijitali
huria akawekeza pesa ya kukuza
Ubuntu
, nakala ya Debian. Aliunda Taasisi ya Ubuntu inayoendelea kukuza programu hiyo huria
[3]
.
Shuttleworth alipata umaarufu wa kimataifa aliporushwa kwenye anga-nje
tarehe
25 Aprili
2002
. Alilipa dolar milioni 20 akasafiri kama
abiria
kwenye
chombo cha anga-nje
cha
Kirusi
Soyuz TM 34 akafika kwenye
Kituo cha Anga cha Kimataifa
(ISS) alipokaa
siku
7 na kushiriki katika
majaribio
ya
kisayansi
. Kutoka kwenye anga-nje aliongea na
rais
Thabo Mbeki
,
Nelson Mandela
na
binti
wa Afrika Kusini Michelle Foster aliyekuwa na miaka 14 akipambana na
kansa
[4]
. Michelle alikuwa na
ndoto
ya kuwa mwanaanga, hivyo akapewa nafasi ya kuongea na Mandela na Shuttleworth kabla hajaaga
dunia
.
- ↑
VeriSign Buys South Africa's Thawte for $575 Million
Archived
22 Juni 2011 at the
Wayback Machine
., tovuti ya internetnews.com ya December 23, 1999
- ↑
"Tovuti ya Shuttleworth Foundation"
. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka
chanzo
mnamo 2014-09-16
. Iliwekwa mnamo
2019-05-28
.
- ↑
Ubuntu carves niche in Linux landscape
, tovuti ya cnet.com ya 21 Juni 2006, kupitia web.archive.org
- ↑
Nelson Mandela Chats With Shuttleworth
, taarifa ya Associated Press ya 2 Mei 2002, kupitia web.archive.org
|
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mark Shuttleworth
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|