Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mapokeo ya Mitume
ndiyo yale yote ambayo
Yesu
aliwakabidhi
Mitume wake
, na kwa
uwezo
wa
Roho Mtakatifu
yatadumu hata
mwisho wa
dunia
katika mafundisho,
liturujia
na
maisha
ya
Kanisa
.
“Nawasifu, kwa sababu mmenikumbuka katika mambo yote, nanyi mmeyashika yale mapokeo vilevile kama nilivyowatolea… Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe” (
1Kor
11:2; 15:3).
“Ilinde ile amana nzuri kwa Roho Mtakatifu akaaye ndani yetu… Mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine” (
2Tim
1:14; 2:2). Tukikata huo mnyororo wa mapokeo, hata kama ni kwa kisingizio cha kushikilia
Biblia
, tunaachana na
asili
ya Kanisa. “Basi, ndugu, simameni imara, mkayashike mapokeo mliyofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wetu… Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu” (
2Thes
2:15; 3:6).
|
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Mapokeo ya Mitume
kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|