Malaika
katika
imani
ya
dini
mbalimbali, kama vile
Uyahudi
,
Ukristo
na
Uislamu
, ni
kiumbe
wa
kiroho
tu anayeweza kutumwa na
Mungu
kwa
binadamu
.
Kwa
umbile
lake hawezi kujulikana na
hisi
za
mwili
wetu.
Katika
Biblia
hawa tu wanatajwa kwa
jina
maalumu:
malaika Mikaeli
,
malaika Gabrieli
na
malaika Rafaeli
(huyo katika
Deuterokanoni
tu).
Katika Uislamu ni kiumbe chepesi ambacho kimeumbwa kwa
nuru
, nacho huwa hakanyagi chini kama mwanadamu, bali huelea juu au kuketi ndani ya
moyo
wa mwanadamu.
Katika Biblia, malaika na watu ndio viumbe pekee vyenye
hiari
ya kuchagua wenyewe wachangie mpango wa Mungu au la. “Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; basi, chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako; kumpenda Bwana, Mungu wako, kuitii sauti yake, na kushikamana naye; kwani hiyo ndiyo uzima wako” (
Kumb
30:19-20).
Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya
milele
. “Kulikuwa na vita mbinguni: Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; nao hawakushinda, wala mahali pao hapakuonekana tena mbinguni” (
Ufu
12:7-8). Chaguo letu binadamu linafanyika
siku
kwa siku kwa kuchukua misimamo mizuri au mipotovu kuhusu
dini
na
maadili
. “Mwayachunguza Maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake; na hayo ndiyo yanayonishuhudia. Wala hamtaki kuja kwangu mpate kuwa na uzima” (
Yoh
5:39-40).
Kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango: alitaka malaika wasioonekana wamtumikie kwa kutusaidia sisi watu, na vile vinavyoonekana tuvitumie kwa
uadilifu
ili kwa njia yetu vimtukuze yeye. “Atakuagizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote” (
Zab
91:11). “Kwa Hekima yako ulimwumba mwanadamu, ili avitawale viumbe vilivyoumbwa nawe, na kumiliki ulimwengu katika utakatifu na kwa haki” (
Hek
9:2-3).
Malaika ni
roho
tupu walioumbwa na Mungu ili wamtukuze milele, wamlinde kila mtu na kumtumikia
Bwana
Yesu
katika kutuokoa. “Angalieni, msidharau mmojawapo wadogo hawa, kwa maana nawaambia ya kwamba malaika zao mbinguni sikuzote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni” (
Math
18:10).
|
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|