Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maisha ya Bikira Maria
kadiri ya
historia
yanajulikana hasa kutokana na habari zilizomo katika
Injili
nne
zinazotumiwa na
Wakristo
pamoja na
Matendo ya Mitume
.
Humo tunasikia jinsi
Bikira Maria
:
- alivyokuwa ameposwa
na
Yosefu
(
Math
1:18),
- alivyopashwa habari na
malaika Gabrieli
kwamba ameteuliwa na
Mungu
kumzaa
Yesu
na alivyoitikia kwa
imani
na
utiifu
huko
Nazareti
(
Lk
1:26-39),
- alivyosafiri haraka ili kumhudumia
Elizabeti
kwa
muda
wa miezi mitatu (Lk 1:30-56),
- alivyokwenda kuishi na Yosefu bila
mahusiano ya kimwili
(Math 1:24-25),
- alivyosafiri naye kwa ajili ya
sensa
(Lk 2:1-5),
- alivyomzaa Yesu karibu na
Bethlehemu
na kumvika
nguo
za kitoto na kumlaza horini (Lk 2:6-18),
- alivyotafakari sana habari za Mwanae (Lk 2:19, 51),
- alivyomtoa kwa Mungu katika
hekalu la Yerusalemu
siku
arubaini
baadaye (Lk 2:22-38),
- alivyomuonyesha kwa
mamajusi
kutoka
mashariki
na kupokea
zawadi
zao (Math 2:11),
- alivyokimbia
Misri
kwa
usalama
wa
mtoto
(Math 2:13-15),
- alivyorudi
Palestina
baada ya
kifo
cha
mfalme
Herode Mkuu
(Math 2:19-21),
- alivyokwenda kuishi tena Nazareti (Math 2:22-23; Lk 2:39, 51),
- alivyokuwa akienda
kuhiji
Yerusalemu
hasa kwa
Pasaka
(Lk 2:41),
- alivyopotewa na Mwanae kwa siku tatu huko Yerusalemu alipokuwa na
umri
wa miaka kumi na miwili (Lk 2:42-50),
- alivyoshiriki
arusi ya Kana
pamoja na Mwanae na kumuomba awasaidie wanaharusi kufanikisha
sherehe
(2:1-11),
- alivyomfuata Kapernaumu (Yoh 2:12),
- alivyomtembelea Yesu akiwa katika mizunguko ya
utume
wake (
Mk
3:31),
- alivyosimama chini ya
msalaba wa Yesu
na kukabidhiwa naye
mtume Yohane
kama mwana (
Yoh
19:25-27),
- alivyokwenda kuishi naye (Yoh 19:27),
- alivyodumu katika
sala
na Wakristo wa kwanza katika kumuomba
Roho Mtakatifu
awashukie (Mdo 1:14).
Habari nyingine zinapatikana katika
Injili ya Yakobo
na
maandishi
mengine, ikiwemo
Kurani
, tena katika
mapokeo
ya
Kanisa
, lakini hazikubaliwi na wote.
Kuhusu suala la Maria kuzaa watoto wengine, katika
Biblia ya Kikristo
hakuna habari hiyo; ingawa wanatajwa
ndugu wa Yesu
, yeye tu anaitwa "mwana wa Maria" (Mk 6:3).
|
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Maisha ya Bikira Maria
kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|