Katika
Ukristo
maadili ya Kimungu
ni yale yanayotokana na
Mungu
na kumwezesha
binadamu
kuhusiana naye inavyotakiwa, yaani kwa:
Kwa maadili hayo, yale
ya kiutu
yanakuwa hai na bora, kwa mfano wa
Yesu Kristo
. Kadiri ya
Kanisa Katoliki
, tofauti na yale ya kiutu, maadili ya Kimungu hayawezi kupatikana kwa juhudi anazofanya mtu, bali kwa
neema
tu: yanamiminiwa rohoni, yaani katika
akili
na katika
utashi
.
Maadili ya Kimungu ni ma
adili
ya kumiminiwa yanayomhusu
Mungu
mwenyewe aliye lengo letu kuu. Tofauti na hayo,
maadili
ya kiutu yanahusu njia za kufikia lengo hilo.
Kati ya maadili ya Kimungu,
imani
inatuwezesha kusadiki yale yote ambayo Mungu
ametufunulia
, kwa kuwa ndiye
ukweli
wenyewe. Ni kama hisi ya Kiroho inayotuwezesha kusikia
muziki
safi wa Kimungu usiojulikana kwa njia nyingine yoyote. Kuna tofauti kubwa kati ya kusoma
Injili
kihistoria au kitaalamu na kuiamini kama
Neno la Mungu
, kwa kuwa kusadiki ni tendo linalopita
umbile
letu na la
malaika
, likituingiza katika
ulimwengu
wa juu. “Kwa maana mmeokolewa kwa
neema
, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na
nafsi
zenu, ni kipawa cha Mungu” (
Ef
2:8). Ndiyo msingi wa kufanywa waadilifu, kwa kuwa inatujulisha lengo lipitalo maumbile tunalopaswa kulikusudia. “
Ibrahimu
alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa
haki
” (
Mwa
15:6;
Rom
4:3,9). “Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; bali na kwa ajili yetu sisi tutakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua
Yesu
Bwana
wetu katika wafu” (Rom 4:23-24). Sisi
tutaokoka
tu kwa imani hiyo ambayo ni
zawadi
ya Mungu.
Kanisa
lilitamka rasmi dhidi ya
Wapelajiupande
kwamba hata mwanzo wa imani ni neema. Imani hiyo inapita kabisa maumbile, si kama
muujiza
unaoonekana au kama
utabiri
wa tukio la kawaida tu (k.mf. mwisho wa
vita
); kwa sababu imani inamhusu Mungu mwenyewe katika maisha yake ya ndani, ambayo hayawezi kujulikana kimaumbile, tena kwa sababu tunasadiki kwa kutegemea
mamlaka
ya Mungu aliyejifunua, ambayo pia haiwezi kujulikana na maumbile. Imani inatufanya tushike kwa namna ipitayo maumbile na isiyoweza kukosa, yale ambayo Mungu ametufunulia kadiri tunavyofundishwa na Kanisa lililokabidhiwa ufunuo huo.
“Tazama, msomi fulani anachimba mafundisho ya Kikatoliki bila ya kuyakataa kwa
ukaidi
, bali anakariri, ‘
Heri
nyinyi mlio na imani; mimi pia ninapenda kuwa nayo lakini siwezi’. Anasema ukweli: anataka asiweze (bado); kwa sababu kusoma na kuwa na nia njema hakufikii daima kujua ukweli, ili ionekane wazi kuwa
hakika
ya
akili
si hakika kuu inayotegemeza mafundisho ya Kikatoliki… Kinachotokea ndani mwetu tunapoamini ni tukio la
mwanga
wa ndani unaopita umbile letu... Mwongofu atawaambia, ‘Nilisoma, nilitafakari, nilitaka nisifike; lakini siku fulani, siwezi kusema vipi, kwenye pembe ya njia, au nyumbani karibu na
moto
, sijui, sikuendelea kuwa yuleyule, nimesadiki... Kilichotokea ndani mwangu katika
nukta
ya kupata hakika kuu ni jambo tofauti kabisa na yale yote yaliyotangulia’. Mwakumbuke wanafunzi wale wawili waliokwenda
Emau
” (
Henri Lacordaire
).
Imani tunayomiminiwa ni kama uwezo wa kusikia ambao unapita maumbile na kutufanya tusikilize
sauti
ya Mungu kupitia
manabii
na
Mwanae
mwenyewe, kabla hatujakaribishwa kumuona
uso
kwa uso. Mtu anayesoma Injili bila ya imani, na mwingine mwenye imani, ni tofauti kama watu wawili wanaosikiliza
wimbo
fulani, lakini mmojawao ana
karama
ya muziki, mwingine hana. Wote wanasikia
noti
zote, lakini yule wa kwanza tu anaelewa undani na
ujumbe
wa wimbo ule. Vivyo hivyo mwamini tu, hata kama hajui kusoma, anashika Injili namna ipitayo maumbile kama Neno la Mungu, wakati msomi pamoja na
elimu
yake yote hawezi kuishika hivyo pasipo imani ya kumiminiwa. “Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo
ushuhuda
ndani yake.
Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa
mwongo
, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe” (
1Yoh
5:10). Miaka mia iliyopita mtu angeshangaa kuambiwa siku moja ataweza kusikia kwa
redio
muziki unaochezwa wakati huohuo katika
nchi
nyingine. Kwa imani ya kumiminiwa tunasikia muziki wa mbinguni, ambao baadhi ya nyimbo zake ni ma[[fumbo ya
Utatu
,
umwilisho
,
ukombozi
,
ekaristi
na
uzima wa milele
. Kwa kusikiliza hayo tunaongozwa zaidi na zaidi kule unakotokea muziki huo bora.
Ili tuelekee kweli lengo hilo na kulifikia, tumepewa mabawa mawili,
tumaini
na
upendo
. Pasipo hayo tunaweza kuelekea tu tunapoelekezwa na akili yetu; kumbe tukiwa nayo tunarukia tunapoelekezwa na imani. Kama vile akili yetu pasipo mwanga wa imani haiwezi kujua lengo letu lipitalo maumbile,
utashi
wetu pia hauwezi kuelekea lengo hilo
nguvu
zake zisipozidishwa na kuinuliwa kwenye ngazi ya juu. Kwa tumaini tunatamani kumpata Mungu, na kusudi tumfikie tunategemea si nguvu za umbile letu, bali
msaada
aliotuahidia, yaani yeye aliye tayari daima kusaidia. Upendo unatufanya tumpende Mungu namna bora zaidi, isiyojitafutia
faida
; si tu ili tumpate hapo baadaye, bali kwa ajili yake na kuliko tunavyojipenda, kutokana na
wema
wake usio na mipaka, unaopendeza kuliko
fadhili
zake zote. Unatufanya tumpende hasa kama
rafiki
aliyetangulia kutupenda. Unamuelekezea vitendo vya maadili mengine yote ukiyahuisha na kuyafanya yaweze kustahili. Ndiyo nguvu yetu kuu ipitayo maumbile, nguvu ya upendo ambayo wakati wa
dhuluma
imeshinda vipingamizi vyote, hata katika viumbe dhaifu kama watakatifu
Anyesi
na
Lusia
. Hivyo mwenye mwanga wa imani anamuelekea Mungu kwa mabawa ya tumaini na upendo. Akitenda
dhambi ya mauti
, mara anapoteza
neema
inayotia utakatifu na upendo, kwa kuwa anajitenga na Mungu akiacha kumpenda kuliko nafsi yake. Hata hivyo
huruma
ya Mungu inamuachia imani na tumaini (mpaka atakapotenda dhambi dhidi ya maadili hayo) awe bado na mwanga wa kumuelekeza njia, na aweze bado kutegemea huruma isiyo na mipaka ili kuomba neema ya
uongofu
.
Kati ya maadili hayo ya Kimungu, upendo ndio la juu zaidi, nao utadumu
milele
pamoja na neema inayotia utakatifu, ambapo badala ya imani na tumaini mtu atakuwa na Mungu akimjua waziwazi, bila ya
hofu
ya kupotewa naye. “Upendo haupungui neno wakati wowote; bali ukiwapo
unabii
utabatilika; zikiwapo
lugha
, zitakoma; yakiwapo
maarifa
, yatabatilika… Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo (
1Kor
13:8,13). Ndio
utendaji
wa juu wa
muundo wa Kiroho
: maadili matatu ya Kimungu ambayo yanastawi pamoja, halafu maadili ya kiutu yanayoendana nayo.