Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu
ya Lorenzo (mnamo 1555-1565).
Lorenzo de' Medici
(
tamka me-di-chi;
1 Januari
1449
-
9 Aprili
1492
) alikuwa
mfanyabiashara
na
mwanasiasa
katika
mji
wa
Firenze
(kwa
Kiingereza
: Florence)
nchini
Italia
wakati wa
karne ya 15
. Aliitwa pia na
watu
wa mji wake
Lorenzo il Magnifico
(Lorenzo adhimu)
[1]
. Lorenzo alizaliwa katika
familia
ya
Medici
waliokuwa wafanyabiashara
tajiri
na
babu
yake
Cosimo de' Medici
aliwahi kupanda ngazi kuwa
mtawala
wa Firenze.
Firenze ilikuwa wakati ule
dola-mji
na
jamhuri
ya kujitegema iliyokuwa tajiri kutokana na
biashara
yake ya kimataifa; ilikuwa
kitovu
cha
kiuchumi
ambako
benki
za kwanza za
Ulaya
zilipoundwa.
Utajiri
wa mji uliwezesha
taasisi
za
elimu
na
kazi
ya
wasanii
wengi, na familia ya Medici ilikuwa kati ya wafadhili mashuhuri zaidi wa elimu na
sanaa
wakati wa
Zama za Mwamko
.
Lorenzo alitumia utajiri wake kuwa
kiongozi
halisi wa
siasa
ya Firenze ingawa hakuchaguliwa katika
ofisi
yoyote
[2]
. Wakati wake viongozi waliochaguliwa katika halmashauri ya
serikali
ya jamhuri hiyo walimtegemea kifedha na kisiasa. Anajulikana zaidi kwa ufadhili wake wa wasanii mashuhuri kama vile
Sandro Botticelli
na
Michelangelo Buonarroti
. Ufadhili huo na
ujenzi
wa
majengo
mazuri kama
makanisa
na majumba ulikuwa sababu ya kumwita "il magnifico" (mwadhimu).
Lorenzo mwenyewe alikuwa pia msanii aliyetunga
mashairi
. Alizaa
watoto
10 na mmojawao aliyeitwa Giovanni akawa
Papa Leo X
.
- ↑
Kent, F.W. (2006). Lorenzo De' Medici and the Art of Magnificence. USA: JHU Press. p. 248.
ISBN 0801886279
.
- ↑
Guicciardini, Francesco (1964). History of Italy and History of Florence. New York: Twayne Publishers. p. 8.
- Miles J. Unger,
Magnifico: Maisha ya kipaji na nyakati za vurugu za Lorenzo de Medici
(Simon na Schuster 2008), wasifu wa Lorenzo.
- Christopher Hibbert,
Nyumba ya Medici: Kuibuka na Kuanguka kwake
(Morrow-Quill, 1980); historia ya jumla ya familia.
- FW Kent,
Lorenzo de- Medici na Sanaa ya Ukubwa (The Johns Hopkins Symposia in Comparative History
(The Johns Hopkins University Press, 2004); muhtasari wa uhusiano wa Lorenzo na sanaa.
- Peter Barenboim,
Michoro ya Michelangelo - Ufunguo wa Tafsiri ya Medici Chapel
(Moscow, Letny Sad, 2006) .
|
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Lorenzo de' Medici
kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|