Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Longitudo
(
ing.
: longitude)
katika ramani au mchoro wa dunia ,ni njia ya kuonyesha mahali duniani kwa kutaja umbali wake kutoka mstari wa
meridiani ya sifuri
kwa kipimo cha digrii (
°
).
Kwenye ramani za kawaida ni mistari inyochorwa kutoka juu hadi chini, ni mistari inayounanisha ncha ya kaskazini na kusini.
Kwenye msingi wa digrii 360 za duara digrii hizi za latitudo huehesabiwa hadi +180° (kwenda mashariki) au hadi -180° (kwenda magharibi). Ni kawaida vilevile kutaja tofauti kati ya longitudo za mashariki au magharibi kwa kuongeza herufi za "E" (east) na "W" (west) badala ya +/-. Pamoja na kipimo cha
latitudo
inataja kamili kila mahali duniani.
Meridiani ya 0° imekubaliwa ni mstari kutoka
ncha ya kaskazini
hadi
ncha ya kusini
unaopita katika mji wa
Greenwich
(karibu na
London
/
Uingereza
).
Digrii za longitudo hugawiwa katika umbali wa 60
dakika
au minuti; dakika hugawiwa katika
nukta
au sekondi. Umbali huu hauna kipimo kamili cha urefu kwa sabau ya umbo la dunia. Kwenye ikweta umbali kati ya longitudo ni 111 km, katika ncha penyewe ni sifuri kwa sababu longitudo zote hukutana hapa.
Mji wa Kiafrika karibu kwenye longitudo ya sifuri ni
Accra
(
Ghana
). Vipimo vyake ni : 5°30' N (latitudo) na 0°10' W (longitudo).