Liege (kwa Kiwallonia Lidje , Kiholanzi Luik , Kijerumani Luttich ) ni mji mkubwa wa jimbo la Wallonia katika nchi ya Ubelgiji . Kuna wakazi 194,000 na wengi wao ni wasemaji wa lugha ya Kifaransa. Kuanzia 972 hadi 1795 ilikuwa mji mkuu wa utemi ndani ya Dola Takatifu la Kiroma uliotawaliwa na maaskofu wa Liege.