Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Lance Henriksen
|
![](//upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/thumb/a/aa/Lance_Henriksen_cropped.jpg/200px-Lance_Henriksen_cropped.jpg) Henriksen mnamo 2010
|
Amezaliwa
|
Lance James Henriksen
5 Mei
1940
(
1940-05-05
)
(umri 84)
New York City
, New York,
U.S.
|
Kazi yake
|
Mwigizaji, Mwigizaji Sauti Mkongwe
|
Miaka ya kazi
|
1961 ? mpaka sasa
|
Ndoa
|
Jane Pollack (1995-mpaka sasa)
|
Lance James Henriksen
(amezaliwa
5 Mei
1940
) ni mwigizaji wa filamu, msanii, anayefahamika zaidi na wapenzi wa TV kwa uhusika wake kwenye filamu za aina ya
bunilizi ya kisayansi
,
aksheni
na za kutisha kama vile
The Terminator
, na
Alien
, na kwenye kipindi cha TV kama vile
Millennium
.
Henriksen alizaliwa mjini
Manhattan
,
New York City
katika familia ya watu maskini kabisa. Baba yake alikuwa baharia wa
Kinorwei
na mwanamasumbwi aliyeitwa jina la utani la "Icewater" ambaye alitumia nusu ya maisha yake akiwa baharini tu. Mama'ke Henriksen alihaha kutafuta kazi akiwa kama mwelekezi wa wanengeaji, mhudumu, na mwanamitindo.
[1]
[2]
Wazazi wake walitalikiana akiwa na umri wa miaka miwili na alilelewa na mama'ke. Kadiri akuanvyo, Henriksen amejikuta akiingia katika matata mbalimbali wakatu yungali shuleni na kuthubu hata kuchungulia majumbani kwa watoto wenzi wake. Henriksen aliondoka nyumbani na kuachilia mbali shule akiwa na umri wa miaka kumi na miwili; hakujifunza kusoma mpaka alivyofikisha umri wa miaka 30, pale alipojiunza mwenyewe namna ya kusoma miswaada andishi ya filamu.
[3]
Ametumia ujana wake mwingi akiwa kama mtoto wa mtaani huko mjini New York. Kutembea na matreni ya mzigo nchi nzima, pia aliwekwa jela kwa makosa madogo kama vile ya uzururaji. Kilikuwa kipindi chake cha bahati kukutana na marafiki zake wa zamani Bw.
James Cameron
na
Bruce Kenselaar
.
Kazi ya kwanza ya Henriksen ilikuwa kwenye tamthilia na alifanya kazi kama mwandalizi wa eneo la igizo; kwa kweli, alipokea uhusika wake kwa sababu alitengeneza seti nzima ya maandalizi. Mwanzoni mwa miaka yake ya 30, Henriksen alihitimu elimu yake ya uigizaji katika chuo cha
Actors Studio
na kuanza kuigiza huko mjini New York City.
[4]
Katika filamu, ameanza kuonekana kwa mara ya kwanza kwenye filamu ya
It Ain't Easy
mnamo mwaka wa 1972. Henriksen akaenda kucheza katika nyusika mbalimbali na filamu pia. Nyusika hizo ni pamoja na kucheza kwenye filamu ya
Steven Spielberg
Close Encounters of the Third Kind
(1977) na
Damien: Omen II
(1978). Pia amewahi kucheza kama mwanaanga
Walter Schirra
kwenye filamu ya
The Right Stuff
(1983) na mwigizaji
Charles Bronson
kwenye filamu ya TV mnamo 1991 -
Reason for Living: The Jill Ireland Story
.
Lance Henriksen akicheza kama Charles Bishop Weyland kwenye
Alien vs. Predator
(2004)
Wakati
James Cameron
anatunga filamu ya
The Terminator
(1984), alipanga hasa uhusika wa Terminator uchezwe na Henriksen. Cameron alikwenda mpaka akachora picha ya Terminator kwa kutumia sura ya Henriksen. Bila kujali, uhusika hatimaye ukaenda kwa
Arnold Schwarzenegger
. Henriksen ameonekana kwenye filamu, alicheza kwenye uhusika mdogo wa Detective Hal Vukovich. Henriksen huenda akawa anafahamika zaidi kwa kucheza kama roboti mwenye mwonekano wa binadamu,
Bishop
, kwenye filamu ya
Aliens
(1986, filamu nyingine ya Cameron) na
Alien 3
(1992). Baadaye kaja kucheza kama Charles Bishop Weyland, mwonekano wa mtu uliotokana na Bishop wa awali, katika
Alien vs. Predator
(2004).
- Ryan's Hope
(1980) - Preston Post
- Tales from the Crypt
(1990) - Reno Crevice
- Millennium
(1996-1999) - Frank Black
- The X-Files
(1999) - Frank Black
- IGPX: Immortal Grand Prix
(2005) - voice of Andrei Rubley
- Caminhos do Coracao
(2007) - Dr. Walker
- Transformers: Animated
(2008-2009) - voice of Lockdown
- NCIS
(2009) - Sheriff Clay Boyd
- Verizon Droid Commercial (2010)
WikiMedia Commons