Mose akipokea Torati (juu) na kuwasomea Waisraeli (chini).
Mose akitazama toka mbali nchi ya ahadi, Kum 34:1-5 (mchoro wa Tissot).
Kumbukumbu la Sheria
(pia:
Kumbukumbu la Torati
) ni kitabu cha tano katika
Tanakh
(yaani
Biblia ya Kiebrania
) na cha
Agano la Kale
katika
Biblia ya Kikristo
.
Kama
vitabu
vingine vyote vya
Biblia
, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa
historia ya wokovu
ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya
ufunuo
wa
Mungu
kwa
binadamu
.
Kwa asili kimeandikwa katika lugha ya
Kiebrania
, na katika
lugha
hiyo kinaitwa
?????????
,
Devarim
, maana yake “Maneno”, ambalo ni
nomino
ya kwanza katika kitabu hicho.
Maelezo yaliyomo ni kama marudio ya sheria iliyotolewa katika
Mlima Sinai
, kwa hiyo kitabu kimeitwa Kumbukumbu la Torati. Jina hilo linatokana na maneno ya
Kigiriki
'deuteros' (maana yake 'ya pili'), na 'nomos' (maana yake 'sheria') yaliyounganika na kuwa
Δευτερον?μιον
,
Deuteronomion
. Ndivyo kilivyoitwa na waliotafsiri Biblia ya Kiebrania mara ya kwanza katika lugha ya
Kiyunani
, miaka 200 hivi
K.K.
(tafsiri yao inaitwa
Septuaginta
).
Kwa kweli kitabu hiki kinapitia upya matukio ya
wokovu
ya wakati wa Musa kikifaidika na ujumbe wa ma
nabii
, hasa
Hosea
. Kwa msingi huo, kitabu hiki kinasisitiza sana
uaminifu
kwa
sheria
za
Agano la Kale
na pia tuzo na adhabu zitakazotolewa kufuatana na matendo ya Waisraeli, lakini pia
upendo
wa Mungu unaodai kurudishiwa.
Wengine wanakiita
Kitabu cha Tano cha
Mose
(au Musa)
kwa vile mapokeo yalimdhania kuwa mwandishi wa kitabu hicho. Siku hizi kitabu hicho kinafikiriwa kuwa kiliandikwa kama miaka 600 baada ya Musa, ingawa kina namna ya
hotuba
alizoweza kuwatolea Waisraeli kabla hajafa.
Vitabu hivyo vitano pamoja kwa jina la Kigiriki vinaitwa
Pentateuko
.
Kitabu cha Kumbukumbu la Sheria kina sura thelathini na nne, ambazo karibu zote zinasimulia hotuba za Mose kwa
Waisraeli
. Mahali ni tambarare ya
Moabu
na wakati ni mwezi wa 11 katika mwaka wa mwisho wa matembezi ya
Wanaisraeli
.
- Hotuba ya kwanza (sura 1 hadi 4) yarudia matokeo muhimu ya safari ya jangwani ya watu wa Israeli. Inaeleza jinsi ilivyo muhimu kumtii
Mungu
. Kuna maonyo dhidi ya
uasi
.
- Hotuba ya pili (sura 5 hadi 26) ni sehemu kuu ya kitabu. Humo kuna marudio ya
Amri Kumi
, sheria kwa ajili ya maisha katika
nchi ya ahadi
na sura ya 20 ina sheria kuhusu
vita
.
- Hotuba ya tatu (sura 27 hadi 30) inajadili yale yatakayofuata kama watu hupuuza maagizo ya Mungu au kuyatekeleza. Mwishoni
ahadi
kati ya Mungu na Wanaisraeli inarudiwa na
Yoshua
ateuliwa kuwa
kiongozi
mpya baada ya Musa.
Ni sura nne za mwisho tu zinazohusu mambo ya kihistoria: Yoshua kuteuliwa
mwandamizi
wa Mose kama kiongozi wa taifa (Kumb 31:1-8 inasimulia jinsi Musa alivyomuachia Yoshua uongozi wa Waisraeli wote kwa kumwekea mikono =
Hes
27:12-23), Mose kuimba
wimbo
wake wa mwisho (sura 32),
baraka
ya Mose kwa
makabila 12 ya Israeli
(sura 33), na mwishoni habari za
kifo
chake Mose (sura 34).
Musa alifikia mpakani mwa
nchi takatifu
asikubaliwe kuiingia kama
adhabu
ya makosa yake, ila alionyeshwa yote kutoka mlimani (Kumb 32:48-52) halafu akafariki (Kumb 34). Kazi aliyopangiwa iliishia huko, mwingine akampokea na kuendeleza
ukombozi
wa Kimungu.
Binadamu
wote ni vyombo tu vinavyotumika kwa muda fulani, halafu vinaweza kuachwa. Kumbe Mungu ndiye mtendaji mwenyewe ambaye hasinzii wala halali, bali anazidi kuwashughulikia watu wake. Kwa
imani
hiyo mtu anatakiwa kuwa daima tayari kuwaachia wengine nafasi yake.
Katika maneno yake yote ya kukumbukwa ni hasa yale ya 6:4-9 ambayo Mwisraeli yeyote anayakariri kila siku katika
sala
na kuyashika pengine
neno
kwa neno.
Maneno mengine muhimu sana yapo 26:5-10: ni kama
kanuni ya imani
ambayo Mwisraeli alikuwa anaiungama mbele ya
Mungu
wakati wa kumtolea malimbuko ya
ardhi
. Hivyo alikuwa akikiri amepewa yote na
Bwana
, halafu akaweza kuyafurahia
mavuno
.
Baada ya kupokea sheria katika
Mlima Sinai
, Waisraeli walikuwa
jangwani
kwa muda wa karibu miaka 40, wakitangatanga kati ya Sinai na
Kanaani
.
Katika muda huo watu wote waliokuwa na umri wa miaka 20 na zaidi wakati wa kuondoka Mlima Sinai walikufa, na kizazi kipya kilikuwa kimepata umri wa kutosha.
Kwa hiyo Musa alirudia kueleza sheria kwa watu wa kizazi hicho, kabla hawajavuka
Yordani
na kuingia
Kanaani
.
Maelezo hayo yalitolewa katika majuma mawili ya mwisho wa maisha ya Musa, Waisraeli walipokaa katika nchi tambarare ya
Moabu
, wakifanya maandalizi ya mwisho ya kuingia Kanaani (
Hes
22:1; 35:1; Kum 1:1-5).
Kurekebisha sheria na kuthibitisha agano
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Kitabu cha Kumbukumbu si marudio tu ya maagizo na amri zilizotolewa hapo awali, bali kina maelezo mengi ya ziada. Kinataja upya amri za sheria, lakini kinatia mkazo zaidi katika maneno mengine.
Sheria zilizoandikwa katika vitabu vya Kutoka, Walawi na Hesabu zilitoa amri kama madai ya moja kwa moja tu, lakini kitabu cha Kumbukumbu, kwa sababu hakikutaka kutoa mafundisho juu ya vitabu vile tu, kinaongeza kueleza kwamba uhusiano wa Waisraeli na Mungu wao lazima uwe zaidi kuliko sheria na madai ya
haki
tu. Uwe uhusiano wa kiroho wenye
upendo
na baraka.
Hali ya kitabu hiki ni ya mfano wa
mhubiri
kuliko wa mtoaji wa sheria, na wasomaji wake au wasikilizaji wake ni watu kwa jumla, kuliko ma
kuhani
na
waamuzi
tu (Kum 8:5-6; 10:12-13).
Kitabu kinasisitiza kwamba, watu watimize
amri za Mungu
ili kumjua na kumpenda Mungu wao zaidi, si kwa sababu tu wamedaiwa kuzitimiza katika maagano (Kum 6:3, 5-9; 7:7-8,11).
Agano
ni msingi wa kitabu, lakini uhusiano baina ya Mungu na watu wake katika agano hilo ulitakiwa uwe wa upendo. Upendo mkuu wa Mungu kwa watu wake usababishe upendo wa kumtii Yeye (Kum 5:6-7; 6:1-3).
Kwa
neema
yake Mungu alichagua Israeli kuwa
taifa
lake akawaahidi kuwapa nchi ya Kanaani iwe nchi yao hasa (Kum 7:6-7; 8:1; 9:4-5).
Kama watu walitaka kufurahia baraka za agano hilo katika
ushirika
wa upendo na Mungu, walipaswa kujua
sheria
yake na kuitimiza. Kizazi kilichotangulia kiliapa kuwa na
uaminifu
katika agano kwa Mungu huko Sinai (
Kut
24:7-8), lakini walikosa vibaya sana. Wakati huo kizazi kipya kilipokuwa tayari kuingia Kanaani, agano lilithibitishwa. Musa alirudia maneno yote ya sheria, na watu waliahidi upya kuitii (Kum 26:17-18).
Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kina mambo mengi yanayofanana na
hati
za maagano jinsi yalivyofanyika katika nchi za maeneo yale hapo kale, ambapo bwana mkubwa au mfalme fulani alifanya mapatano na watu waliokuwa chini yake au waliomtegemea. Maagano kama hayo hayakutokana na
majadiliano
ya makundi mawili yaliyokuwa sawa, bali yalikuwa kadiri yaliyoandaliwa na yule mkuu, yakitangaza
mamlaka
yake juu ya watu na kupanga
kanuni
za maisha yaliyowapasa. Watu hawakuwa na njia yo yote ila kukubali masharti ya mkuu au ya mfalme wao.
Kwa kawaida hati ya agano ilianza kwa
utangulizi
wa
historia
ambapo mkuu alijieleza akiorodhesha mambo yote aliyowafanyia watu wake. Kisha ikafuata orodha ya masharti ya maagano yaliyowekwa juu ya watu. Kwanza, watu walionywa kuwa waaminifu na watiifu kwa mkuu wao, na baadaye walionywa wasianzishe
fitina
yo yote kwa kufanya
mapatano
na mfalme mwingine. Baada ya masharti yale ya msingi, amri na sheria zake zilielezwa kinaganaga zilizohusika na matakwa ya sehemu ile.
Kwa kawaida katika hati hizo ma
shahidi
walitajwa. Pia zilieleza
faida
ambazo zitatokana na
utiifu
wa watu na adhabu ambazo zitatokana na uasi. Kisha hati ilifungiwa na kutunzwa kwa usalama katika
patakatifu
pa watu waliohusika, ili iweze kusomwa wakati wowote, na hapo iweze kupata nyongeza zake kama zikitakiwa.
Mara nyingine hati ilimalizika kwa kujumlishwa
muhtasari
wa maagizo na masharti maalumu, au kwa ahadi kwamba maagano hayo yaendelee kwa muda wote ambao watu wataendelea kuwa waaminifu na watiifu kwa masharti yake.
Kuhusu agano baina ya Mungu na Israeli alama nyingi za namna hiyo zinaonekana katika maandiko ya sheria zilizoandikwa katika vitabu vya
Kutoka
, Kumbukumbu la Torati na katika
kitabu cha Yoshua
. Kitabu cha Kumbukumbu la Torati kimeandikwa kwa mtindo ulioelezwa hapo juu.
Licha ya mpangilio wa kitabu kwa jumla kufanana na hati za maagano kama zilivyoandikwa katika nchi zile wakati ule, hata mambo mengi yanayoshughulikiwa katika maagano hayo yanaonekana sehemu mbalimbali katika kitabu hicho.
1:1-4:43 Utangulizi wa historia
4:44-11:32 Maagizo ya msingi kuhusu agano
12:1-26:19 Amri zote zatajwa kinaganaga
27:1-30:20 Masharti ya agano
31:1-34:12 Siku za mwisho za Musa
Vitabu vinavyofuata Kumbukumbu la Sheria
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Vitabu vinavyofuata katika
Biblia ya Kiebrania
(Yoshua, Waamuzi, Samweli na Wafalme) vinataka kuthibitisha kwamba kweli ikawa kama hiki kinavyosema: Waisraeli walipofuata agano (wakati wa
Yoshua
) waliteka
nchi ya ahadi
na kuifurahia, lakini walipozidi kuasi (wakati wa
Waamuzi
,
Samweli
na
Wafalme
) walikuja kunyang’anywa nchi ile yote, kwanza sehemu nzuri zaidi (
kaskazini
), halafu ile hafifu zaidi (
kusini
). Hapo Waisraeli wote wakajikuta tena utumwani katika nchi ya kigeni kama kabla ya Musa, wakikosa hata
sanduku la agano
, lililopotea wakati wa maangamizi ya
Yerusalemu
na
hekalu
lake, baada ya wao kufikia hatua ya kula watoto wao kutokana na njaa.
Vitabu hivyo vilikamilishwa wakati wa kukaa uhamishoni
Babeli
, vikiwa jibu la swali kuu lililowakwaza huko: je,
Mungu
wetu ameshindwa? Waandishi walichagua matukio mbalimbali ya
historia
baada ya Yoshua ili kuthibitisha kuwa aliyeshindwa ni Israeli, si Mungu. Historia hiyo inaonyesha mfululizo wa maasi hata baada ya Mungu kutuma waamuzi na manabii wake ili kuwaonya Waisraeli na kuwaelekeza upya.
Lengo la waandishi halikuwa kutunza kumbukumbu za mambo yote kwa usahihi na ukamilifu, bali kuelekeza njia ya kupata
wokovu
hata baada ya Israeli kuonekana imekoma moja kwa moja. Kama vile
Biblia
nzima, vitabu hivyo vinalenga wokovu wetu, vikihakikisha kuwa Mungu anaweza kuleta mwanzo mpya hata hali ikiwa mbaya namna gani. Ndiyo sababu habari ya mwisho kabisa ni ya kuleta
tumaini
: kwamba
mfalme Yekonia
alitolewa gerezani (alipokaa miaka 37) na kufanywa mgeni wa kudumu mezani pa mfalme wa Babeli.
- Miller, Patrick D (1990).
Deuteronomy
. Cambridge University Press.
- Phillips, Anthony (1973).
Deuteronomy
. Westminster John Knox Press.
- Avigdor Miller
(2001).
Fortunate Nation:Comments and notes on DVARIM
.
- Block, Daniel I (2005). "Deuteronomy". Katika Kevin J. Vanhoozer (mhr.).
Dictionary for Theological Interpretation of the Bible
. Baker Academic.
- Bultman, Christoph (2001). "Deuteronomy". Katika John Barton, John Muddiman (mhr.).
Oxford Bible Commentary
. Oxford University Press.
- Christensen, Duane L (1991). "Deuteronomy". Katika Watson E. Mills, Roger Aubrey Bullard (mhr.).
Mercer Dictionary of the Bible
. Mercer University Press.