Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Koloni
ni
neno
linalotumiwa kwa kutaja:
- makazi mapya ya watu kutoka eneo moja katika eneo jingine
- eneo linalotawaliwa na nchi ya mbali hasa kwa kusudi la kufaidi
malighafi
yaliyopo au kwa shabaha ya kuwa na
kituo cha kijeshi
au cha
biashara
.
Asili ya neno koloni ni
Kilatini
"colonia" kutokana na
kitenzi
"colere" (kulima, pia kuabudu). Colonia ilikuwa makazi ya
Waroma wa Kale
nje ya eneo lao la awali. Chanzo chake kilikuwa
mji
mpya uliokaliwa na
wanajeshi
wastaafu waliopewa
ardhi
kwa ajili ya
mashamba
kama
pensheni
yao.
Makoloni ya aina hiyo yalianzishwa hasa mpakani mwa maeneo mapya yaliyotwaliwa karibuni na kungizwa katika
Dola la Roma
.
Walowezi
walipewa mashamba yao kwa masharti ya kuwa tayari kutetea mipaka kama vita inatokea.
Makoloni yalienea hasa tangu upanuzi wa nchi za
Ulaya
kuanzia
karne ya 15
kwa maana ya maeneo yaliyo chini ya nchi nyingine ambayo iko mbali. Makoloni hayo yalianzishwa kwa njia mbalimbali:
- Makoloni mengine yalianzishwa kwa kusudi la kulima
mazao
au kupata malighafi yasiyopatikana walikotokea wakoloni. Mfano wake ni
Peru
ambako
Hispania
ilijipatia kwa wingi
madini
ya
fedha
. Mfano mwingine ni
visiwa vya Karibi
vilivyogeuzwa kuwa mashamba ya
miwa
kwa mahitaji ya
sukari
ya Ulaya.
- Makoloni yaliundwa tena kwa shabaha ya kupeleka walowezi huko. Mfano wake ni makoloni ya
Uingereza
katika
Amerika Kaskazini
yaliyounda baadaye nchi ya
Marekani
. Mengine yaliundwa kwa kusudi la kuwapeleka wafuasi wa
madhehebu
ya
dini
yasiyopendwa Uingereza penyewe au kwa shabaha ya kuwapeleka huko watu
maskini
waliokosa mashamba kwao.
Australia
ilianzishwa kama koloni la wafungwa wa
magereza
waliopelekwa mbali ili kuwaondoa nyumbani.
Hasa mwisho wa
karne ya 19
nchi za Ulaya zilitwaa maeneo na kuyafanya makoloni kwa
hofu
ya kwamba nchi nyingine itayachukua. Kuwa na koloni kulikuwa kama
dalili
ya kuwa nchi yenye maana inayoheshimiwa. Mwisho wa karne hiyo takriban 80
%
za maeneo yote
duniani
yalitawaliwa kama koloni la namna moja au nyingine.
Kipindi hiki cha
ukoloni
kiliporomoka baada ya
vita kuu ya pili ya dunia
, ila kukawa na mwendelezo wake katika
ukoloni mamboleo
.
Koloni kamili, eneo la kudhaminiwa na nchi lindwa
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Hali za nchi chini ya
utawala
wa kikoloni zilitofautiana.
- Kwa upande mmoja palikuwa na makoloni yaliyotawaliwa moja kwa moja na watawala wa nje.
- Baada ya
Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
aina mpya ya koloni ilitokea iliyoitwa
eneo la kudhaminiwa
. Nchi tawala ilikuwa na mamlaka juu ya koloni kwa niaba ya
Shirikisho la Mataifa
(League of Nations mandates), baadaye na
Umoja wa Mataifa
(Unites Nations trust territories). Maeneo ya kudhaminiwa yalikuwa kiasili chini ya nchi zilizoshindwa wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia yaani
Ujerumani
na
Uturuki
na kuhamishwa chini ya utawala wa nchi washindi kama Uingereza, Ufaransa,
Ubelgiji
na
Japani
. Tofauti na koloni la kawaida ilikuwa katika masharti ya kutoa taarifa kwa Umoja wa Mataifa na katika utaratibu wa kupata uhuru.
Tanganyika
ilikuwa eneo la kudhaminiwa mikononi mwa Uingereza kuanzia mwaka 1922 baada ya kuanzishwa kama koloni la Kijerumani.
- Kwa upande mwingine palikuwa na nchi na maeneo ambako watawala wenyeji waliendelea kuwa na
madaraka
fulani lakini walipaswa kushauriana na wawakilishi wa nchi kubwa. Nchi hizo zilitazamwa mara nyingi kama “
nchi lindwa
”
(protectorate)
chini ya
ulinzi
wa Uingereza,
Ufaransa
na kadhalika. Viwango vya mamlaka vya watawala wenyeji vilikuwa tofauti. Mara nyingi zilikuwa kama koloni za kawaida tu ilhali mamlaka halisi zilikuwa mkononi mwa mwakilishi wa mkoloni aliyetoa maagizo kwa jina la mfalme au sultani mwenyeji.
Zanzibar
ilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza.
Kuna mifano ambapo hali ya kuwa nchi lindwa ilidumu muda mfupi tu kabla ya kumezwa kabisa na kuwa sehemu ya koloni kamili. Mfano wake mmojawapo ni
usultani
wa
Witu
ulioingizwa katika koloni la
Kenya
bila kujali mawazo ya mtawala mwenyeji au ya watu wake.
Lakini kuna pia mifano ambapo
mikataba
asilia na wenyeji iliheshimiwa na mwisho wa ukoloni maeneo haya yamekuwa
nchi huru
. Kati ya mifano yake ni
Falme za Kiarabu
na
Botswana
iliyokaa nchi ya pekee nje ya
Afrika Kusini
ingawa
serikali
ya Afrika Kusini ilitaka iwe chini yake.
Kwa jumla Uingereza ulipendelea mara nyingi kutawala kupitia wenyeji kuliko kuwatawala moja kwa moja. Utawala wa moja kwa moja ulipendelewa kwa mfano na Ufaransa katika makoloni yake.
|
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Koloni
kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|