Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mifano
|
- Oliver '
hakutaka
kula
ugali
- Habibu
angali
anasoma
darasani
- Sisi
tunataka
kwenda
kuogelea
mtoni
|
Kitenzi kikuu kisaidizi
(alama yake ya
kiisimu
ni:
TS
) ni
kitenzi
ambacho hukaa sambamba na
kitenzi kikuu
ili kukisaidia kukamilisha taarifa. Kitenzi kikuu kisaidizi kikiwa peke yake hakiwezi kutoa taarifa kamili. Hivyo basi ni lazima kiambatane na kitenzi kingine (kikuu) ndipo taarifa yake ikamilike.
- Babu yangu
alikuwa
anaumwa
sana (
alikuwa
ni kitenzi kisaidizi
TS
- na
anaumwa
ni kitenzi kikuu
T
).
- Wezi
walikuwa
wanataka
kuiba
fedha zake (
walikuwa
na
wanataka
vyote ni vitenzi visaidizi - isipokuwa
kuiba
ambapo hapa kimeainishika kama kitenzi kikuu). Kwa kawaida kitenzi kikuu hukaa mwisho hata kama nyuma yake kutakuwa na wasaidizi kumi.
- Anna
alikuwa
anataka
kwenda
kununua
matunda sokoni (
alikuwa
,
anataka
, na
kwenda
vyote ni vitenzi visaidizi isipokuwa
kununua
inabaki kuwa kitenzi kikuu
- Upepo
ulikuwa
umesha
ezua
mabati yote
- Juma
hakuwa
anataka
kwenda
kununua
matunda sokoni
Angalizo
: Kitenzi kikuu alama yake ni
T
kubwa na kitenzi kisaidizi alama yake ni
TS
.
Dhima za kitenzi kikuu kisaidizi
[
hariri
|
hariri chanzo
]
Dhima za kitenzi kikuu kisaidizi zimegawanyika katika makundi makuu mawili - nayo ni:
1) Kujulisha
njeo
(njeo = wakati, nyakati)
2) Kujulisha uyakinishi na ukanushi wa tendo/matendo
Sifa za Kitenzi kisaidizi
- Hakikamilishi taarifa. Mfano, Baba
alikuwa
- Mara zote huambatana na kitenzi kikuu katika kutoa taarifa. Mfano, Upepo
ulikuwa
unavuma.
- Hudokeza nyakati mbalimbali za kutendeka kwa tendo. Yaani, wakati uliopo, uliopita na ujao. Mfano, Alikuwa, Atakuwa, n.k
|
Makala hii kuhusu mambo ya
lugha
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kitenzi kikuu kisaidizi
kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|