Kitabu cha Hagai
ni kimojawapo kati ya
vitabu
12 vya
Manabii wadogo
ambavyo, pamoja na vingine vingi, vinaunda
Tanakh
, yaani
Biblia ya Kiebrania
. Hivyo ni pia sehemu ya
Agano la Kale
katika
Biblia ya Kikristo
.
Kama vitabu vingine vyote vya
Biblia
, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa
historia ya wokovu
ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya
ufunuo
wa
Mungu
kwa
binadamu
.
Kazi ya
nabii
huyo kati ya
Agosti
na
Desemba
ya
mwaka
520
KK
, wakati uleule alipoanza
nabii Zekaria
, ni mwanzo wa kipindi cha mwisho cha
unabii
katika
Israeli
kabla ya ujio wa
Yohane Mbatizaji
na
Yesu Kristo
.
Kabla ya
uhamisho wa Babeli
,
ujumbe
wa manabii ulitishia mara nyingi
adhabu
ya
Mungu
kwa
uasi
wa
taifa
lake.
Wakati wa
uhamisho
ujumbe ulikuwa wa faraja zaidi.
Ule wa Hagai na Zekaria ulilenga
ustawi
wa
Wayahudi
waliokuwa wamerudi
Yerusalemu
mwaka
538 K.K.
ili kujenga upya
hekalu
, lakini walichelewa kutekeleza azma yao, kutokana na upinzani na mahangaiko ya kujipatia
riziki
katika
mazingira
magumu.
Mbaya zaidi, walikaribia kukata tamaa. Kwa changamoto ya manabii wao,
gavana
Zerubabeli
na
kuhani mkuu Yoshua
waliongoza wananchi kukazania
ujenzi
huo na kuukamilisha mwaka
515 KK
.
Juhudi hizo ndizo lengo la
hotuba
zote
nne
zinazounda kitabu hiki, ambapo ujenzi wa hekalu ni sharti la ujio wa
ufalme wa Mungu
.
Ahadi
ya kuwa hatimaye hekalu jipya litakuwa tukufu kuliko lile la
Solomoni
ni la maana zaidi kwa
Wakristo
wanaoiona kama
utabiri
wa
Yesu
mfufuka
, aliye hekalu la kweli la
Agano Jipya
(
Yoh
2:19-22).
|
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kitabu cha Hagai
kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|