Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kismayu
(pia:
Kismayo
au kwa
Kisomali
:
Kismaayo
) ni
mji
katika
mkoa
wa
Jubbada Hoose
wa
Somalia
mwambaoni mwa
Bahari Hindi
. Uko karibu na
mdomo
wa
mto
Juba
. Kismayu ndio mji mkubwa katika eneo la Jubbaland. Mji wenyewe uko
km
528
kusini
magharibi
mwa
mji mkuu
Mogadishu
.
Katika
mwaka
wa
2011
, Kismayu ilikadiriwa kuwa na wakaazi 183,300
[1]
.
Mji ulianzishwa na
Wabajuni
waliokuwa
Waswahili
Wabantu.
Wasomali
wenyewe walichelewa kufika eneo hili.
Katika karne za kati, Kismayu ilikuwa chini ya serikali ya
Ajuuraan
iliyokuwa ikutawala eneo kadhaa za
Somalia
.
Kismayu pamoja na pwani ilikuwa chini ya masultani wa
Zanzibar
tangu
1835
BK
. Kati ya
1875
na
1876
Kismayu ilitawaliwa na
Misri
.
Tangu
1895
ilikuwa chini ya utawala wa
Uingereza
pamoja na
Kenya
lakini mwaka
1924
ilikabidhiwa kwa utawala wa
Italia
. Ikawa mji mkuu wa jimbo la
Oltre Giuba
(ng'ambo ya Juba).
Kismayu iliharibika sana kutokana na mapigano katika
vita vya wenyewe kwa wenyewe
vya Somalia tangu 1991.
- ↑
"SOMALIA City & Town Population Geography Population Map cities coordinates location - Tageo.com". www.tageo.com. Retrieved 23 December 2016.
|
Makala hii kuhusu maeneo ya
Somalia
bado ni
mbegu
.
Je unajua kitu kuhusu
Kismayu
kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|