Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mita hii katika gari ni tayari kuonyesha kasi kwa km/h
Kilomita kwa saa
(
kifupi
:
km/h
) ni
kipimo
cha
kasi
.
Km
peke yake ni kifupi cha
kilomita
na
h
ni kifupi cha
saa
(kutoka
Kilatini
hora >
Kiingereza
hour)
.
Kitu
chenye kasi ya km/h 1 (kilomita
moja
kwa saa) kinatembea kilomita moja katika
muda
wa saa moja.
Mwanadamu
kwa mwendo wa
wastani
anatembea kwa km/h 5 yaani katika muda wa saa moja anatembea kilomita tano. Kwa kutumia
baisikeli
kwa kasi ya wastani mtu husafiri kwa km/h 15 hadi km/h 20.
Magari
yanaruhusiwa kusafiri kwa 50 km/h
mijini
na 80 hadi km/h 100 nje ya miji.
Kipimo cha
SI
kwa kasi ni
m/s
yaani
mita
kwa
sekunde
lakini hakitumiki sana kwa sababu katika
maisha
ya kila siku watu hawataki kujua mwendo wao kwa kila sekunde.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
sayansi
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kilomita kwa saa
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|