Kibodi
(pia:
Kiibodi
[1]
, Kicharazio
[2]
,
Baobonye
au
Bodidota/Bodi ya dota
[3]
; kwa
Kiingereza
:
keyboard
) ni
kifaa
muhimu kinachomwezesha
mtu
kuweka
maandishi
na
namba
kwa
tarakishi
(kompyuta). Inafanywa na vibonye vingi kwa ajili ya kila
herufi
na alama nyingine zinazotumiwa mara kwa mara.
Kibodi ni pia sehemu ya chombo cha
muziki
k.v.
piano
, iliyo na vibonye vyenye
rangi
vinavyobonyezwa ili kutoa
sauti
.
Kwa tarakilishi nyingi ni kifaa kikuu cha kuingizia habari
mashineni
.
Kuna mifumo mbalimbali za baobonye kulingana na
lugha
.
Muundo
wa kawaida kwa lugha zinazotumia
alfabeti ya Kilatini
ni
QWERTY
(hizi ni
herufi
6 za kwanza).
Muundo huu unaweza kuchosha
mikono
na
vidole
. Ulianzishwa zamani za
mashine za kupiga chapa
na mfumo wa
herufi
ulilenga kutovurugisha mikono ya taipu. Siku hizi ni kama hakuna taipu tena, lakini watu waliozoea muundo umebaki vile.
Kibodi ni kifaa cha kuingiza data kwenye kompyuta au vifaa vingine vya elektroniki kwa kutumia herufi, namba, na alama nyingine. Historia ya kibodi inaanzia katika miaka ya mapema ya karne ya 19 wakati ilianza kutumika kwa mashine za kuchapa.
Mashine za kwanza za kuchapa zilikuwa zikitumia kibodi za mekaniki ambazo zilikuwa na
herufi
zilizopangwa kwa njia ya kawaida. Mfano maarufu wa kibodi za awali ni
Sholes and Glidden Typewriter
ambayo ilizinduliwa mwaka
1873
.
Kibodi za kisasa zilianza kujitokeza katika miaka ya
1960
na
1970
, wakati
teknolojia
ya
umeme
ilianza kuchukua nafasi ya mifumo ya
mekaniki
. Kibodi za
kompyuta
za kwanza zilikuwa na muundo wa kawaida wa
QWERTY
, ambao bado unaendelea kutumika hadi leo.
Kwa miaka mingi, kibodi kimekuwa kifaa muhimu sana katika
kompyuta
na vifaa vingine vya
elektroniki
. Limekuwa likiboreshwa na kubuniwa upya mara kwa mara ili kuboresha ufanisi na urahisi wa matumizi. Leo, kibodi za kompyuta zina vifungo maalum kwa ajili ya kazi mbalimbali kama vile kupiga simu, kurekebisha sauti, au kufikia huduma za
mtandao
.
- ↑
KKS
Kamusi Kuu ya Kiswahili, toleo la nne, TUKI 2019
- ↑
Kamusi Kuu ya Kiswahili
- ↑
Kamusi ya Karne ya 21, EMAC, BAKITA na KIE. ISBN: 998-702-097-6