Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kebo ya umeme
Kebo ya baharini ya mawasiliano
Kebo
(kutoka
Kiing.
cable
) ni muunganisho wa
nyaya
zilizofunikwa kwa mpira au
plastiki
ambazo hutumiwa kupitishia
umeme
,
simu
, au
ishara
za
nuru
[1]
.
Kazi ya kebo ni ama kubeba
nishati
au ishara za habari.
Nyaya za kupitisha umeme kwa kawaida ni za
shaba
,
alumini
au
aloi
za
metali
. Kebo za kupitisha
data
siku hizi hutumia hasa
nyuzi za kioo
zinazopitisha ishara za nuru.
Nyaya ndani ya kebo ni lazima kutengwa kwa
vihami
kati yake vinavyozuia kuingiliana kwa mikondo ya umeme au ishara za habari
[2]
.
Kama kebo inayoathiriwa na nguvu za nje inahitaji kuimarishwa.
Marejeo