한국   대만   중국   일본 
Katekisimu ya Kanisa Katoliki - Wikipedia, kamusi elezo huru Nenda kwa yaliyomo

Katekisimu ya Kanisa Katoliki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katekisimu ya Kanisa Katoliki (kwa kifupi KKK ) ni kitabu rasmi cha kufundishia dini ya Ukristo kadiri ya imani na maadili ya Kanisa Katoliki kutokana na Mtaguso wa pili wa Vatikano .

Ilikubaliwa na Papa Yohane Paulo II kwanza tarehe 11 Oktoba 1992 , halafu moja kwa moja 15 Agosti 1997 .

Katika mtandao inapatikana katika lugha zifuatazo:

Vitabu vilivyotangulia [ hariri | hariri chanzo ]

Vitabu vya kufundishia dini ya Kikristo vilitolewa kuanzia Mababu wa Kanisa , lakini neno maalumu katekisimu lilianza kutumiwa na Martin Luther mwaka 1529 .

Wakati wa Mtaguso wa Trento ilitolewa katekisimu kwa ajili ya ma paroko ili waweze kufundisha vizuri imani katoliki. Katekisimu ya Trento ilipitishwa na Papa Pius V ikaenea katika Kanisa Katoliki lote.

Baada yake, hakukuwa na katekisimu nyingine ya kimataifa, ingawa kuanzia mwaka 1905 ilienea sana ile iliyoandikwa na Papa Pius X kwa jimbo la Roma .

Walengwa [ hariri | hariri chanzo ]

Katekisimu ya Kanisa Katoliki inatarajiwa kutumika hasa kama msingi kwa utunzi wa katekisimu za kila lugha na aina kadiri ya mahitaji ya watu.

Yaliyomo [ hariri | hariri chanzo ]

Katekisimu ya Kanisa Katoliki ina sehemu kuu nne:

Mafundisho yote yanaendana na madondoo mengi, hasa ya Biblia , Mababu wa Kanisa , Mitaguso ya kiekumene , Ma papa na watakatifu .

Ufupisho Makini [ hariri | hariri chanzo ]

Papa Benedikto XVI , ambaye alipokuwa kardinali (Joseph Ratzinger) aliongoza utunzi wa KKK, mwaka 2005 alitoa Ufupisho wake, uliotafsiriwa katika Kiswahili kwa jina la Ufupisho Makini .

Katika mtandao anapatikana kwa lugha mbalimbali, k. mf. kwa Kiingereza: Compendium of the Catechism of the Catholic Church