Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kasi
ya
gimba
ni
umbali
uliotembewa nalo kwa
muda
fulani. Gimba lenye kasi kubwa linapita njia kwa muda mdogo; kama kasi yake inapungua gimba litahitaji muda zaidi kwa njia hiyohiyo. Kasi ni
kipimo
cha
mwendo
wa
kitu
.
Katika
fizikia
alama
ya kasi ni
v
(kutoka
Kilatini
velocitas
).
Hesabu
yake hufuata
fomula
Kasi "v" ni umbali "d" gawa kwa
wakati
"t":
Kuongezeka kwa kasi huitwa
mchapuko
(au mchapuo, kwa
Kiingereza
:
acceleration)
. Kupungua kwa kasi ni
mchapuohasi
(kwa Kiingereza:
deceleration
).
Mfano:
Gari
linatembea kwa muda wa
saa
moja
bila kikwazo chochote kwa mwendo usiobadilika. Kama limepita njia ya kilomita 80 katika kipindi hiki tunasema kasi ya gari ni
kilomita
60 kwa
saa
au 60
km/h
.
Kipimo sanifu cha SI
kwa kasi ni
mita
kwa
sekunde
(m/s).
Kwa miendo ya kila
siku
, hasa ya
vyombo vya usafiri
, kipimo cha kawaida ni km/h.
Katika nchi zinazotumia kipimo cha
maili
kuna pia maili kwa saa.
- mtu kwa mwendo wa wastani hutembea kwa kasi ya 5 km/h.
- baisikeli hufikia kasi ya 20 km/h.
- gari linalotembea mjini kwa kawaida kuruhusiwi kupita kasi ya 50 au 60 km/h.
- nje ya mji magari huruhusiwa kutembea hadi kasi ya 100 km/h katika Kenya na Tanzania
- mwanamichezo anayekimbia sana hufikia kasi hadi 37 km/h kwa mufa mfupi
- mnyama wa nchi kavu mwenye kasi kubwa ni
duma
mwenye kasi ya 110 km/h
- gari la moshi lenye mbio mkubwa nchini Japani hufikia kasi ya 350 km/h
- ndege kubwa za abiria hutembea kwa mwendo wa 850 km/h
- dunia
yetu (pamoja na viumbe vyote juu yake) huwa na kasi ya kilomita 107,280 kwa saa ikizunguka jua.
- mwendo mkubwa ulimwenguni ni
kasi ya nuru
inayopita kilomita 299,792 kwa kila sekunde.
Tofauti na kasi (kwa Kiingereza:
speed
) ni
kasimwelekeo
(pia: velositi; ing.
velocity
); hiyo inataja kasi pamoja na mwelekeo wake. Alama yake ni
.
|
Makala hii kuhusu mambo ya
fizikia
bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu
Kasi
kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuongeza habari
.
|