Mt. Karolo wa Sezze alivyochorwa.
Karolo wa Sezze
(
Sezze
, leo katika
wilaya
ya
Latina
,
Italia
,
19 Oktoba
1613
-
Roma
,
6 Januari
1670
), alikuwa
bradha
wa shirika la
Ndugu Wadogo
Wareformati
aliyeandika vizuri sana kuhusu
maisha ya kiroho
.
Anaheshimiwa na
Kanisa Katoliki
kama
mtakatifu
.
[1]
Alitangazwa kwanza
mwenye heri
na
Papa Leo XIII
mwaka
1882
, halafu mtakatifu na
Papa Yohane XXIII
tarehe
12 Aprili
1959
.
Sikukuu
yake huadhimishwa tarehe ya
kifo
chake, 6 Januari, au kesho yake
[2]
.
Jina
la kuzaliwa lilikuwa Giancarlo Marchioni. Tangu
utotoni
alilazimika kujitafutia riziki akahimiza wenzake kumuiga
Yesu
na watakatifu wake
[3]
. Alipokuwa
kijana
alitamani kwenda
India
kama
mmisionari
.
Kisha kuvutwa na maisha ya watakatifu mabradha
Wafransisko
Paskali Baylon
na
Salvador wa Horta
, aliamua kujiunga na shirika lao, alipokubaliwa mwaka
1635
.
Baadaye alieleza kuwa alifanya hivyo ili kuishi kifukara na kuombaomba "kwa upendo wa Kristo".
[4]
Pia alikuwa na heshima ya pekee kwa Yesu
Ekaristi
[5]
.
Karolo aliishi katika
jumuia
mbalimbali kama bradha, asiombe kamwe
upadrisho
: alikuwa
mpishi
,
bawabu
,
mtunzasakristia
,
mtunzabustani
na ombaomba. Kwa kukosa
ufundi
katika
kazi
hizo zote, alijulikana kwa sababu ya kuuunguza
jiko
zima.
[4]
Akiwa bawabu, siku moja alikatazwa na
mlinzi
wa jumuia asitoe
chakula
kwa wasio
watawa
. Karolo
alitii
, lakini mara moja misaada iliyotolewa kwa jumuia ilipungua sana. Hapo alimsaidia mlinzi kutambua uhusiano kati ya mambo hayo mawili. Aliporuhusiwa tena kusaidia
maskini
, misaada kwa jumuia iliongezeka tena.
[4]
Ingawa hakuwa
padri
, Karolo aliagizwa na
muungamishi
wake kuandika habari za maisha yake. Ndivyo kilivyopatikana
kitabu
Makuu ya Rehema za Mungu
ambacho kilienea na kusomwa sana.
Vilevile alipaswa kutoa mashauri ya kiroho kwa watu mbalimbali akaandika vitabu vya namna hiyo.
Papa Klementi IX
alipokuwa mahututi alimuita ili kupata
faraja
na
baraka
yake.
[4]
|
Makala hii bado ni
mbegu
.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa
kuihariri na kuiongezea habari
.
|